24.8 C
Dar es Salaam
Friday, October 4, 2024

Contact us: [email protected]

Mtoto aliyeibia Songea apatikana Moshi alikouzwa kwa Sh 30,000

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Gemini Mushy, akiwa amembeba mtoto wa umri wa miezi mitano (5) ambaye aliibwa akiwa na umri wa siku saba katika Kijiji cha Likalangiro kilichopo Halmashuri ya Madaba mkoani humo na alipatikana Februari 18 mwaka huu katika kijiji cha Kokirie wilaya ya Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro.

AMON MTEGA, SONGEA

MTOTO  Shazira Yahaya  aliyeibiwa akiwa na siku saba katika Kijiji cha Likalangiro Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma, amepatikana  katika Kijiji cha Kokirie Wilaya ya MoshiVijijini mkoa wa Kilimanjaro, ambapo aliuzwa kwa Sh 30,000.

 Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Gemini Mushy,  alisema mtoto huyo ambaye sasa ana miezi mitano, aliibiwa Septemba 26 mwaka 2018 majira ya saa 3:00 na alipatikana Moshi vijijini  Februari 18 mwaka huu.

 Alisema baada ya jeshi hilo kupokea taarifa ya kupotea kwa mtoto huyo kutoka kwa mama mzazi,  Amina Abdalah (17), upelelezi ulianza hadi kufikia  Februari 18 mtoto alipopatikana.

 Mushy alimtaja mtuhumiwa aliyehusika kumuiba mtoto kisha kwenda kumuuza kuwa ni Abrahamu Kilewa (20) mkazi wa kijiji cha Mahanje katika Halmashauri ya Madaba na kuwa alienda kumuuza mtoto huyo kwa Anosiata Luambano (36) ambaye ni mfanyabiashara na ni mkazi wa Marangu Moshi ambaye anadaiwa alimununua kwa Sh 30,000.

“Mtoto huyo aliuzwa kwa Sh 30,000 akiwa ana umri wa siku saba, tumepata baada upelelezi mkubwa ulifanywa na Askari F.2229D/CPL Victor  ambaye alijituma kwa kujitolea uhai wake kwenda kumuokoa mtoto huyo”alisema kamanda Mushy.

 Alisema hadi sasa watuhumiwa wote wanashikiliwa na polisi huku taratibu za mtoto huyo kumkabidhi kwa wazazi wake zikiendelea kufanywa kwa kushirikiana na kitengo cha ustawi wa jamii na kuwa mtoto huyo ana afya njema.

 Akizungumza na MTANZANIA nje ya ofisi hiyo, Askari Victor alisema haikuwa kazi ndogo kwani alipata ajali akiwa kwenye kazi hiyo ambayo mguu mmoja aliumia.

Naye afisa ustawi wa jamii Manispaa ya Songea, Victor Nyenja, alisema ofisi yao imempokea mtoto huyo na yupo kwenye mikono salama na wamejiridhisha kuwa afya yake ni njema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles