28.6 C
Dar es Salaam
Saturday, January 28, 2023

Contact us: [email protected]

MTEULE MWINGINE WA TRUMP AKATAA WADHIFA

WASHINGTON, MAREKANI


MCHUMI ambaye aliteuliwa na Rais Donald Trump, kujaza wadhifa wa Waziri wa Jeshi la Majini, Philip Bilden, amejiondoa baada ya kuonekana kukiuka sheria za taifa kuhusu mgongano wa masilahi.

Bilden, ofisa usalama wa zamani wa jeshi ambaye alitumia miaka 20 akifanya kazi katika kampuni binafsi ya fedha mjini Hong Kong, alieleza kuhusu wasiwasi wa maisha yake ya usiri na changamoto atakazokumbana nazo katika kutenganisha kazi na biashara zake.

“Baada ya mchakato wa kina wa tathimini, nimeamua kwamba sitoweza kuiridhisha Ofisi ya Maadili ya Serikali katika suala la mgongano wa masilahi na biashara za familia yangu,” alisema Bilden katika taarifa.

Awali Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Majini zilikana ripoti za mapema mwezi huu kuwa Bilden angejitoa kutokana na kuwa na sababu sawa na zile zilizosababisha kujitoa kwa Vincent Viola, aliyekuwa chaguo la Trump kusimamia jeshi la Marekani.

Bilionea huyo wa Wall Street alijitoa Februari 3, mwaka huu akieleza sheria kumbana kutokana na biashara za familia yake.

Waziri wa Usalama, Jim Mattis, alisema atampendekeza mtu atakayechukua nafasi ya Bilden katika kipindi cha siku chache zijazo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles