30 C
Dar es Salaam
Friday, January 27, 2023

Contact us: [email protected]

NYUMBA YA MAMA WEMA YAPIGWA MAWE

KYALAA SEHEYE Na BEATRICE KAIZA-DAR ES SALAAM


MAMA mzazi wa mrembo wa Tanzania mwaka 2006 Wema Sepetu,  Mariam Sepetu, usiku wa kuamkia jana nyumba yake iliyopo maeneo ya Sinza Mori jijini Dar es salaam imepigwa mawe juu ya bati kwa muda wa saa moja na nusu.


Akizungumza na MTANZANIA nyumbani kwake jana alisema kuwa usiku wote huo alikosa raha na kupata hofu kubwa na kuhisi kuna watu wabaya ambao walikuwa wanataka kumvamia na kujikuta akikosa usingizi.


“Nimekosa usingizi  na hofu juu huku simu yangu iliishiwa salio kwani nilikuwa nikitaka kupigia simu ndugu na majirani ili waje kunisaidia, sikuweza kutoka nje kwa kuwa sikuwa najua mbaya wangu amekaa wapi na amekusudia kufanya nini,” alisema.
Baada ya kupambazuka alitoa taarifa kwa mwanae Wema na viongozi wengine wa Chadema ambapo Meya wa Ubungo, Boniface Jacob alifika ili kuangalia hali ya mama huyo na kuamua kumuwekea ulinzi.


“Tumeshaangalia mazingira yote tumegudua kitu ambacho hatuta kiweka wazi kwa sasa ila tutaweka ulinzi mkali na atakaye jaribu shauri yake hatuta kubali suala hili liendelee kumkuta kamanda wetu na mimi mara kwa mara nitafika kuangalia mazingira,” alisema Jacob.

Meya alifafanua zaidi kuwa ulinzi huo hautaishia nyumbani kwa mama Wema, bali hata nyumbani kwa Wema ulinzi utaimarishwa, kwa sababu wamegundua wanachama hao wapya wamekuwa wakiwindwa na watu wasiojulikana.
Kwa upande wake Wema alipohojiwa alisema, anashindwa kuelewa  hao  watu waliofanya kitendo hicho walikuwa wanataka nini kutoka kwao.


“Mama yangu ameteseka  usiku kucha kwa kukosa amani, amelia na kukosa hata hamu ya kula tumefika tumemkuta katika hali mbaya, najua yana mwisho ila tutazidi kufanya dua ya kumwomba Mungu atuepushe na mabaya yote,” alisema Wema.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles