23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Mtembee pamoja ili kuleta mabadiliko -Dk Chaula

Mwandishi Wetu- Dodoma

KATIBU Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Zainab Chaula  amewataka watumishi na uongozi wa Hospitali ya Mirembe kuhakikisha wanatembea pamoja kwa kudumisha ushirikiano baina yao ili kuleta mabadiliko chanya, ikiwemo kuboresha huduma zitolewazo na kuboresha stahiki za watumishi katika hospitali hiyo.

Dk. Chaula, aliyasema hayo jana  alipofanya ziara ya kutembelea Hospitali ya Mirembe na kufanya mazungumzo na watumishi ili kujadiliana namna gani watatatua changamoto walizonazo katika maeneo yao ya kazi.

“Tunatakiwa kukaa pamoja na tutembee pamoja wakati wote ili kuleta mabadiliko katika hospitali na taasisi yetu, tuache kulalamika maana sisi sote tulio hapa ndio Serikali yenyewe,” alisema.

Aliagiza uongozi wa hospitali  hiyo kuwa wabunifu kwa kuhakikisha wanasimamia miradi yao vizuri, hali itakayosaidia kuongeza makusanyo ya mapato na kupelekea kuboresha huduma za afya na stahiki za watumishi katika hospitali hiyo.

“Hospitali inatakiwa iwe ya mfano, mnatakiwa kuongeza jitihada na ubunifu katika utendaji wenu, ikiwamo usimamizi mzuri wa miradi, tunataka kuona mabadiliko ili kuweza kusonga mbele,”alisema.

Aliagiza maboresho katika maabara, huku akiahidi kurudi baada ya wiki moja ili kuona maboresho yaliyofanywa, ikiwa ni sehemu ya usimamizi na ufuatiliaji wa maboresho ya huduma zinazotolewa katika hospitali hiyo.

Aliwataka kujiepusha na vitendo vya rushwa ili kutenda haki kwa kutoa huduma kwa usawa kwa wagonjwa wote maeneo ya kazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles