30 C
Dar es Salaam
Saturday, December 4, 2021

Bodaboda aua mwenzake kwa kugombea abiria

Nyemo Malecela – Kagera

BODABODA Mugisha Theonest amepigwa na kusababishiwa mauti baada ya bodaboda mwenzake, Frank Kafumba waliyekuwa wakigombea abiria kumsingizia kuwa  alitaka kumpora pikipiki.

Tukio hilo, lilitokea Machi 3, mwaka huu saa 12 jioni, wakati Mugisha na mwenzake, Erick Cosmas wakiwa wakitoka kupeleka abiria eneo la Ranchi ya Kagoma, wakati wanarudi Kayanga Karagwe ndipo walikuta abiria wengine njiani wakimsubiri Kafumba (bodaboda), aliyekuwa ameitwa kutoka Katagwe na abiria hao lakini amechelewa kufika na kuamua kuwapakia.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi Mkoa  Kagera, Revocatus Malimi alisema wakati Mugisha na Cosmas wakiwa njiani na abiria hao walikutana na Kafumba ambaye alianzisha ugomvi, akidai arudishiwe gharama za mafuta aliyotumia lakini hawakuelewana.

Ndipo mtuhumiwa (Kafumba), aliamua kuwafuata wanakoelekea na walipofika kituo cha mwisho, ugomvi ukawa mkubwa na kuanza kupigana huku bodaboda aliyechukuliwa wateja (Kafumba) aliamua kupiga simu kwa bodaboda wa kijiwe chake kuomba msaada kuwa anataka kuporwa pikipiki yake.

“Baada ya kuomba msaada kwa bodaboda wenzake na wananchi wengine walifika na kuanza kumpiga Mugisha na kumsababishia majeraha yaliyosababisha kulazwa hospitali ya Nyakahanga  kwa ajili ya matibabu lakini kwa bahati mbaya alikuwa ameumia vibaya na kusabisha  kifo chake ambacho kimetokea Machi 5, mwaka huu.

Alisema uchunguzi ulibainika Mugisha na mwenzake, Cosmas hawakuwa wezi au hawakuwa na nia ya kumpora pikipiki Kafumba kama ilivyodaiwa, bali ugomvi wao ulishabanishwa na kugombea abiria,” alieleza Malimi.

Alisema tayari mtuhumiwa amekamatwa na wengine waliohusika  wanaendelea kusakwa ili wachukuliwe hatua kwa kosa la kujichukulia sheria mkononi.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,968FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles