24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

MTATIRO ASHIKILIWA POLISI KWA SAA 29 KWA TUHUMA ZA KUMKASHIFU MAGUFULI

NA AZIZA MASOUD, DAR ES SALAAM

MWENYEKITI wa Kamati ya Uongozi wa Chama cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro, ameachiwa kwa dhamana jana baada ya kushikiliwa kwa saa 29 katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam kwa madai ya kumkashifu Rais Dk. John Magufuli kupitia ukurasa wake wa Facebook.

Hata hivyo, aliachiwa saa 9:30 alasiri jana baada ya kufika kituoni hapo juzi saa nne asubuhi kutokana na kupigiwa simu ya kuhitajika kwa ajili ya kutoa maelezo kuhusu ujumbe aliouandika katika Facebook.

Kushikiliwa kwa Mtatiro kumesababishwa na ujumbe aliouandika Julai 3, mwaka huu kupitia ukurasa wake Facebook uliohusisha  taarifa iliyomuhusu kijana aliyemtaja kwa majina ya Justin Emmauel (31) ambaye ni mkazi wa Misungwi mkoani Mwanza aliyefikishwa mahakamani kwa kosa la kumdhihaki Magufuli.

Kwa mujibu wa Mtatiro alieleza kuwa hati ya mashtaka iliandikwa kuwa kijana huyo  alitamka maneno: “Rais kitu gani bwana.” ambayo polisi walisema ni dhihaka dhidi ya Magufuli.

Maelezo yaliyoandikwa katika hati hiyo ya mashtaka na kuelezwa kuwa ni kosa yalionekana kumshangaza Mtatiro ambaye  chini ya ujumbe huo alirudia maneno hayo yanadaiwa kuwa ni kosa kwa kuandika katika ukurasa wake wa Facebook: “Nami narudia maneno hayo hapa chini, Rais kitu gani bwana.”

Akizungumza gazeti hili kituoni hapo jana, Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF, Mbarala Maharagande, alisema  Mtatiro anatakiwa kuripoti kituoni hapo Jumatatu ya keshokutwa na ameachiwa   baada ya kudhaminiwa na mtu mmoja.

“Nimemdhamini mimi na dhamana haina masharti yoyote zaidi ya kutakiwa kufika kuripoti Jumatatu asubuhi,” alisema Maharagande.

Alisema kabla ya kuachiwa kiongozi huyo alihojiwa na baadaye kutakiwa kutoa neno  la siri la Ipad yake ambalo polisi walilazimika kulifuata nyumbani kwake.

“Tunashukuru ametoka kwa leo (jana) yameshaisha, hapa tunaelekea Mahakama Kuu kuna kesi yetu inaendelea tunaweza tukatoa ufafanuzi zaidi kuhusu hili baadaye,” alisema Maharagande.

Naye Mtatiro hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo kwa jana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles