24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Mtandao wa Asasi za Huduma za kifedha(TAMFI) watangaza washindi 13

Na Mwandishi Wetu Mtanzania Digital

MTANDAO wa Asasi za Huduma za Kifedha (TAMFI) mwishoni mwa wiki wamewatakangaza washindi 13 waliojinyakulia jumla ya Sh milioni 85 katika Tuzo za Ujasiriamali Mdogo za Citi (CMA).

Mkurugenzi Mtendaji wa Citibank Tanzania, Geofrey Mchangila jijini Dar es Salaam akihutubia washindi wa tuzo za mjasiriamali bora wa mwaka wa CITI Micro, 2021 Ijumaa, Julai 16, 2021. Karibu washindi 13 kwa pamoja walichukua nyumbani kama Sh milioni 85. Tuzo hizo mwaka huu zimeunganishwa na Malengo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (UN SDG).

Katika hafla iliyofanyika kwa njia ya mtandao, ushindi wa kwanza katika tuzo hizo ilienda kwa Ruth Gidion Magawa ambaye anamiliki kiwanda kidogo cha kuchakata maziwa alioyejinyakulia dola 7,500 na tuzo ya pili ilenda kwa, Daudi Marko Simfuke mwenye kiwanda cha zana za kuchakata bidhaa za kilimo ambaye alipata dola 6000.

Mshindi wa tatu wa dola 4,000 alikuwa ni Joyce Robert Kalamageambaye ana endesha duka la dawa, zahanati na dukakuu dogo.

Washindi wengine ni Victoria Kavula, Suma Mwanjabiki, Daniel Mpanduzi,Aristides Kenzio,David Mugitu,Richard Kashinje, Tabitha Gityamwi,.Hellena Sailas na Salum Msengi.

Washindi hao 13 walitokana na idadi ya watu 24 walioingia raundi ya mwisho kati ya washiriki 350 waliosajiliwa awali.

Tuzo hizo zimeendeshwa nchini mara ya 4 kwa ushirikiano kati ya Citi Foundation na TAMFI. Tuzo za mwaka huu zimeunganishwa na Malengo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (UN SDG).

Tuzo hizo ni sehemu ya mwendelezo wa benki ya Citi kwenye eneo la mikopo midogo midogo kuwasaidia wajasiriamali wadogo kwa kupitia utoaji tuzo za Citi kwa kila mwaka.Mkakati huo ulianzishwa mwaka 2005 kwa kutambua michango ya wajasiriamali wadogo na pia michango ya asasi zinazotoa huduma za kifedha kwenye maeneo yao.

Mwakilishi wa majaji Prof Jones Kaleshu, alisema kwamba katika msimum huu wameoma mabadiliko makubwa katika ufanisi wa tuzo na pia dhamira safi za washiriki kujiinua kitija.

Alisema tuzo hizo zimeinua molariya wajaioriamali wadogoa ambao wanahitaji msukumo wa pekee kuondojka pale walipo kwa sasa.

Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji MKuu wa Citibank Tanzania, Geofrey Mchangila, program hiyo (CMA) imelenga kutambua mchango wa wajasiriamali hao katika kuimarisha kipato chao kaya zao na taifa kwa ujumla.

Alisema tuzo hizo zimezingatia wajasiriamali wabunifu wanaokwenda sambamba na malengo ya maendeleo endelevu ya umoja wa mataifa.

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TAMFI, Altemius Millinga, ambaye apia ni Mkurugenzi mtendaji wa

Yetu Microfinance Bank PLC, alipongeza program hiyo na kusema inashughulikia kuwapatia mitaji watu wasiokuwa na uwezo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles