23.6 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

MSICHANA ANAYEKULA, LALA NA KUCHEZA NA NYOKA

JOSEPH HIZA NA MASHIRIKA


WATOTO wengi waonapo nyoka hujiwa na mawazo ya kifo, lakini msichana huyu mwenye umri wa miaka 11 nchini India haogopi hilo na huihesabu jamii hiyo ya mijusi hatari kuwa marafiki wake wakubwa.

Msichana huyo, Kajol Khan kutoka Ghatampur, Jimbo la Uttar Pradesh nchini India anaendelea kula na kulala na wanyama hao hatari licha ya kujikuta aking’atwa mara kwa mara.

Anasema: “Nafurahia sana kucheza na cobra. Huniumiza wakati wanaponing’ata, lakini wakati mwingine ni makosa yangu mwenyewe kwa sababu huwachokoza. Inafurahisha.”

Baba wa Kajol, Taj Mohammad, ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 50, alifanya kazi kama mkamata nyoka wa Ghatampur kwa kipindi cha miaka 45.

Tayari amehamisha utaalamu wake huo wa kuwatawala viumbe hao kwa mtoto wake mkubwa wa kiume Gulab (31) na sasa inaonekana Kajol, ambaye ndiye kitinda mimba anaelekea kuendeleza biashara ya familia na kuthihirisha msemo; mtoto wa nyoka ni nyoka!

“Sipendi shule. Napendelea kushughulika na nyoka,”anasema wakati akizungumzia kuhusu elimu.

Ukaribu wake na viumbe hao hatari inamaanisha ndio washirika wake wakuu.

Tangu urafiki wake na wauaji hao uanze ameshang’atwa tumboni, mashavuni na mkononi. Aliugua sana lakini aliweza kupona kabisa.

“Inauma wakati wanaponing’ata lakini huwa hawamaanishi hilo, hujikuta nikiingiwa kidogo na woga wakati ninapoona damu lakini baba yangu huniuguza. Hukimbilia msituni na kuja na dawa.”

Baba wa Kajol kwa sasa ni maarufu katika mkoa wao huo na anaitwa kwa utani kama Bhura, neno lenye maana ya ‘mkamata nyoka.’

Lakini huambulia pauni 14 sawa na Sh 42,000 kwa kukamata nyoka kutoka majumbani na madukani eneo hilo.

“Tunawasaidia watu wa eneo hili na kukamata nyoka walioingia katika nyumba zao,” Taj alisema.

Anaongeza; “Baba yangu ni mkamata nyoka, baba yake alikuwa mkamata nyoka. Ni biashara ya familia yetu na tunajivunia kuifanya.

Dawa hiyo inatokana na majani ya mimea pori, ambayo inabakia kuwa siri kubwa.

Huitengeneza na kuchanganya na saladi na pilipili nyeusi, kisha inaliwa na kusuguliwa katika jeraha.

“Iwapo dawa inawekwa mara moja itakuokoa. Imeniokoa mara nyingi na inaonekana kufanya kazi kwa Kajol pia.

Lakini mama wa Kajol, Salma Bano haonekani kufurahishwa na mwelekeo wa maisha ya bintiye huyo.

Anamuombea maisha nje ya ukamataji nyoka – hasa tangu afukuzwe shule baada ya kwa kuingia darasani na wanyama wake hao wakiwa  katika begi lake la mgongoni.

“Nataka aende shule kama watoto wengine. Iwapo ningekuwa na uwezo ningewaangamiza hawa nyoka lakini anawapenda sana na hivyo sitaki kumvunja moyo,” anasema Salma.

“Kwa sasa amekataa kusoma na hucheza na nyoka siku nzima.

“Najaribu kumfanya asome sana akiwa nyumbani, lakini anaendelea ukaribu na nyoka.'

Taj anasema: “hatuna wageni wengi. Watu hawapendi wanyama wetu nyoka, hivyo wanawafanya wakae mbali nasi kwa vile wanawaogopa.

“Lakini hatujali sana, lakini tunamsikitia Kajol kwa vile watoto huogopa sana kuja na kucheza pamoja naye. Si kama watoto wengine.'

Mama yake mwenye wasiwasi mwingi aliongeza: 'atapata wakati mgumu kupata mume siku za usoni iwapo hataacha kucheza na nyoka wake hao.'

Inakadiriwa kwamba nyoka hao wenye sumu kali wanahusika na vifo vya watu 50,000 kila mwaka duniani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles