26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 27, 2021

LORAINE MAURER: MHUDUMU MWENYE MIAKA 94, ASIYEFIKIRIA KUSTAAFU

JOSEPH HIZA Na MASHIRIKA


AMEUTUMIKIA mgahawa wa Big Macs kwa miaka 44 sasa, lakini mfanyakazi huyo wa McDonald Loraine Maurer (94) hana mpango wa kustaafu karibuni.

Mfanyakazi huyu mwenye bidii ya kazi alijiunga na kampuni hiyo mwaka 1973 huko Evansville katika Jimbo la Indiana nchini Marekani.

Anasema hataki kuondoka kwa vile anaipenda kazi yake hiyo, wafanyakazi wenzake na wateja wake.

Aliwasilisha ombi la kazi katika kampuni hiyo ya fast food ili kupata fedha za ziada baada ya mumewe Kenneth kulazimika kustaafu kutokana na ulemavu alioupata baadaye.

Wakati wa majira ya baridi, wateja waaminifu kwake humpatia lifti ya kwenda na kurudi kutoka kaizini kumsaidia akamilishe shifti yake.

Loraine anasema: “Najua nini kinachoendelea miongoni mwa wateja wangu, najua baadhi ya watoto wao. Baadhi huniomba niwaombee na hufanya hivyo. Najua maisha yao.”

Baada ya mumewe kufariki dunia, mgahawa na wafanyakazi wake na wateja wamekuwa sehemu ya maisha yake na kumsaidia kukabiliana na kipindi kigumu cha huzuni na upweke.

Na kazi ngumu zake na msingi imara wa marafiki waaminifu, ambao ulishuhudiwa na Chip na Katie Kenworthy, ambao wanaumilili mgahawa huo.

Katie alisema: “Loraine ana ufuasi mkubwa. Ana wateja wengi wampendao ambao hufurika katika mgahawa wetu kumuona.

Anasema watu kutoka mji mzima huja kupata kifungua kinywa kilichoandaliwa na Loraine, ambaye huamka saa tisa alfajiri na kuanza kazi saa 11 asubuhi.

Mume wa Loraine alifariki dunia mwaka 1980 hali iliyomfanya kuwa mkiwa lakini kufanya kazi McDonald na kuzungumza na wateja wake, msaada kutoka kanisani na watoto wake wanne kumemsaidia sana kuikabili hali hiyo.

Loraine anasema: “Wao ni waokoaji wa maisha yangu wakati nilipompoteza mume. Wateja wamenisaidia mno.”

 

Wingi wa wateja waliomiminika wakati wa kusherehekea miaka 44 ya kutoa huduma kwake mgahawani hapo ulidhihirisha namna alivyogusa maisha ya wengi.

Bosi Katie anasema: “Baada ya miaka yote hiyo amebakia na dhamira ya kuwatumikia wateja wake kwa ucheshi na moyo wake wote.

 “Loraine ana kundi kubwa la wafuasi, ambao hupenda kuhudumiwa naye wakati wanapoingia katika mgahawa huo wa McDonald.”

Mbali ya kupendelea kuzungumza na wateja, Loraine anafurahia chakula kwa kula McDonald katika kila zamu yake.

Huagiza vyakula pale anapokuwa mgonjwa huku mlo wake aupendao ukiwa ‘sandwich’ ya samaki.

Akiwa na umri wa zaidi ya miaka 90, Loraine sasa anafanya shifti mbili kwa wiki na ana mpango wa kuendelea kwa miaka mingi ijayo.

Anasema: “Nitaikosa sana iwapo nitastaafu na hivyo sitaki kukumbwa na sonona kutokana na upweke. Naifurahia kazi yangu na walionizunguka.”

“Wateja wangu ni sehemu ya maisha yangu. Nimesafiri pamoja nao, kucheza nao, wao si tu ni wateja bali pia marafiki zangu.”

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,388FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles