22.5 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Msiba wa Senga wawakutanisha Lowassa, Nape

NAPENa PATRICIA KIMELEMETA, DAR ES SALAAM

MAHASIMU wa kisiasa, Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa, jana wamekutana kwenye msiba wa aliyekuwa mpiga picha mkuu wa gazeti la Tanzania Daima, Joseph Senga.

Lowassa alifika kwenye viwanja vya TP vilivyopo Sinza ambapo mwili wa marehemu ulikuwa unaagwa saa mbili kamili asubuhi na baadaye Nape aliwasili akiongozana na Katibu Mkuu wake, Profesa Emanuel Ole Gabriel, na moja kwa moja alielekea kwenye viti vya wageni maalumu kwa ajili ya kusubiri kuwasili kwa mwili wa marehemu.

Wakiwa katika eneo hilo, viongozi hao walionekana kujadiliana mambo mbalimbali huku wakiwa wanacheka, jambo ambalo liliwashangaza waombolezaji waliokuwa  kwenye eneo hilo.

Saa tatu asubuhi, Msemaji wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, aliwasli kwenye eneo hilo.

Baada ya kuwasili kwa viongozi hao, mwili wa marehemu ulifikishwa kwenye viwanja hivyo kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho kabla ya kusafirisha kwenda Kijiji cha Shushi kilichopo wilayani Kwimba, Mkoani Mwanza kwa ajili ya mazishi.

Kabla ya kuagwa kwa mwili huo, viongozi mbalimbali walipata nafasi ya kutoa salamu za rambirambi, ambapo Nape aliwataka wanahabari kumuenzi marehemu kupitia picha zake.

Mbali na hao, viongozi wengine walioshiriki kuagwa kwa mpiga picha huyo ni pamoja na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura, Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika. Mwili wa Senga utazikwa leo kijijini kwao Shushi, wilayani Kwimba mkoani Mwanza. Marehemu ameacha mjane na watoto saba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles