21.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 4, 2022

MSHTAKIWA KESI YA BILIONEA MSUYA AACHIWA HURU

Upendo Mosha, Moshi

Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, imemuachia huru mshitakiwa wa nne wa kesi ya mauaji ya mfanyabishara wa madini ya Tanzanite, Bilionea Erasto Msuya, baada ya mahakama hiyo kujiridhisha kuwa hana kesi ya kujibu.

Akitoa uamuzi hayo mahakamani hapo leo Jumatatu Mei 14, Jaji anayesikiliza shauri hilo, Salma Maghimbi, amesema mahakama hiyo imepitia ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka na kujiridhisha kuwa mshtakiwa huyo Jalila Zuberi, hana kesi ya kujibu.

“Ushahidi ulitolewa na upande wa mashtaka katika kesi hii dhidi ya mshtakiwa wa nne hautoshi kumtia hatiani, hivyo mahakama hii inamuachia huru mshitakiwa huyu,” amesema.

Amesema ushahidi uliotolewa mahakamani hapo ni wa mazingira na si wa macho na kwamba hakuna mtu hata mmoja aliyeweza kuona bilionea huyo akiuawa, hivyo mahakama hiyo imezingatia ushahidi huo na kuona mshtakiwa huyo hana kesi ya kujibu.

“Mashahidi wa upande wa mashtaka waliofika mahakamani na kutoa ushahidi wao ni 27 na ushahidi wa maelezo ni mitano hivyo jumla ya mashahidi ni 32 na katika ushaidi wote huu ulioleta na upande wa mashitaka haujatosha kumfanya mshitakiwa awe na kesi ya kujibu,” amesema Jaji Salma.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,654FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles