24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Mshtakiwa azimia mahakamani, wenzake wadai wamenyimwa chakula Keko kwa siku tano

Kulwa mzee -Dar Es salaam

MSHTAKIWA  Habonimana Nyandwi raia wa Burundi, anayekabiliwa na kesi ya mauaji ya Mwanaharakati wa kupambana na mauaji ya tembo, Wayne Lotter amezimia mahakamani wakati kesi yao ilipokuwa ikitajwa  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wakati mshtakiwa huyo akiwa amezimia wenzake wameieleza mahakama hiyo kuwa, raia wa kigeni katika kesi hiyo  wanaoishi Gereza la Keko wamenyimwa chakula kwa siku tano na kusababisha hali yao kudhoofu.

Mshtakiwa Ndimana Zebadayo ambaye ni raia wa Burundi amedai hayo wakati kesi hiyo inayomkabili yeye pamoja na wenzake 17 ilipofika mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa.

Awali Wakili wa Serikali, Esther Martin alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Mfawidhi, Godfrey Isaya kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa kwani upelelezi haujakamilika na jalada la kesi liko kwa DPP.

Kabla washtakiwa hawajapanda kizimbani, mshtakiwa Habonimana Nyandwi raia wa Burundi, alishindwa kusimama na kudondoka chini huku akionekana kugeuza macho, ndipo askari waliokuwa karibu walimsogelea na kumvua viatu na mkanda.

Baada ya kupanda kizimbani mshtakiwa Zebadayo aliomba kuzungumza, aliangua kilio na kudai, raia wa kigeni waliopo  kwenye kesi hiyo hawajui ushiriki wao lakini hawana ndugu wala mtu yeyote wa kuwaona wala kuwapa chakula.

Alidai wamedhoofika hawana ndugu wa kuwapelekea chakula hapa nchini na gerezani wananyimwa chakula na jana ilikuwa ni siku ya tano.

Akijibu hoja hizo, Wakili Esther alidai, mahabusu wanapatiwa huduma zote za chakula pamoja na malazi Magereza, hivyo kuhusu hilo inatakiwa waulizwe Magareza. 

Alidai upelelezi uko hatua za mwisho, jalada lipo kwa DPP kwa ajili ya kulisoma.

Askari magereza alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo za kutopewa chakula alidai kuwa hana taarifa, anachojua yeye mahabusu wote wanapata chakula.

Mshtakiwa Ayubu selemani amedai, katika mahabusu ya keko kuna raia wa kigeni wengi na wote wanapata chakula kwa wakati isipokuwa wawili hao waliopo kwenye kesi hiyo wamekatiwa huduma.

Hakimu Isaya ameahirisha kesi hiyo kwa siku saba, itatajwa tena Januari 24 mwaka huu ili kupata taarifa zaidi juu ya malalamiko ya washtakiwa hao.

Washtakiwa katika kesi hiyo ya mauaji ni raia wa Burundi Habonimana Nyandwi na Nduimana Jonas maarufu Mchungaji (40) mkazi wa Kamenge Burundi. 

Wengine ni Godfrey Salamba (42) mkazi wa Kinondoni Msisiri A. Innocent Kimaro (23) mkazi wa Temeke Mikoroshini, Chambie Ally (32) mkazi wa Kia/Boma na Ofisa wa NBC, Robert Mwaipyana (31) mkazi wa Temeke Mikoroshini.

Wengine ni Meneja wa Benki ya Backlays, Khalid Mwinyi (33) mkazi wa Mikocheni B, Rahma Almas (37) mkazi wa Mbagala B na Mohammed Maganga (61) mchimba makaburi, Allan Mafue, Ismail Mohammed, Leornad Makoye, Amino Sham, Ayoub Selemani, Joseph Lukoa, Gaudence Matemu na Abuu Mkingie.

Katika kesi ya msingi washtakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa kuwa kati ya Julai mosi na Agosti 16, 2017 walikula njama ya kufanya mauaji ya Lotter.

Katika shtaka la pili, washtakiwa hao wanadaiwa Agosti 16, 2017 katika makutano ya barabara za Chole na Haile Selasie iliyopo wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam, wanadaiwa kumuua Lotter

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles