24 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Msako magari yanayopiga ving’ora, kuwasha vimulimuli bila kibali

Ramadhan Hassan, Dodoma

JESHI  la Polisi Mkoa wa Dodoma, limepiga marufuku magari ambayo si ya viongozi wa juu wa Serikali  na yake ya wagonjwa (ambulance) kupiga ving’ola na vimulimuli  huku likisema limekamata magari 27 yakiwemo ya Serikali kutokana na kufanya vitendo hivyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, alisema magari ambayo yatapiga ving’ola tofauti na viongozi wa juu ni lazima yapate kibali maalum.

Alisema jeshi la polisi lilifanya msako na kukamata magari 27 yaliyofungwa ving’ora, vimulimuli, taa zenye mwanga mkali na zenye kubadilisha rangi ikiwa ni kutekeleza agizo lilotolewa hivi karibuni na Mkuu wa Jeshi la Polis nchini, IGP Simoni Siro.

Muroto alisema IGP alishapiga marufuku yote ambayo siyo ya viongozi wa Serikali, ulinzi na usalama, zimamoto au ambulance kutumia alama hizo.

Alisema gari litakaloruhusiwa kutumia ni ambalo  limepata kibali maalumu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

“Magari yaliyokamatwa yana kosa chini ya kifungu 39 (B) (1) (2) na kifungu cha 54(1) (2) (3) (4) na (5) cha sheria ya usalama barabarani sura 168 ya mwaka 1973 na marejeo 2002”, alisema Muroto.

Alisema pia ni mrafuku kujiongezea taa kali za ziada na ni kosa kisheria.

Kamanda huyo aliwataka madereva wote nchini kuzingatia sheria hizo za alama za barabarani kwa kutofunga  taa kali za ziada, vimulimuli na ving’ora  kwa kulinda usalama na uhai wake na wa watu wengine.

Katika hatua nyingine, Muroto alisema  wamefanikiwa  kuwakamata watuhumiwa watatu wakiwa na  lori lenye namba za usajili T 464 CGR ikiwa imepakia Drum 4 za nyaya za umeme aina ya ABC Conductor  zenye ukubwa mita 3200 ambazo zinatumiwa na Shirika la Umeme nchini (Tanesco) kusamabazia umeme.

Alisema walikamata gari hiyo inayodhaniwa imebeba mali ya wizi Julai 15 saa 10 jioni katika Kijiji cha Mbande Kata ya Sejeli Wilaya ya Kongwa katika barabara kuu ya Dodoma.

“Baada ya kufanya uchunguzi wetu tulibaini watuhumiwa hao walikuwa wakisafirisha mzigo huo bila vibali wala risiti za manunuzi, walificha nyaya hizo chini ya mizigo ya bidhaa zingine za matumizi ya nyumbani,’’alisema Muroto.

Muroto aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Ramadhani Mussa (25) mkazi wa Mkuyuni Mwanza, Athuman Abbas (22) mkazi wa Bohari Mwanza na Shafii Mussa (23) Mkazi wa Bohari Mwanza.

Kamanda Muroto alisisitiza watu kuacha kuhujumu Uchumi kwani Serikali inajitahidi kuweka miundo mbinu  kwaa ajili ya kuwanufaisha Wananchi watu wanahujumu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles