25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Takukuru yaokoa milioni za wastaafu waliobambikiwa riba kubwa za mikopo

MURUGWA TOMAS, TABORA

 TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoani Tabora, imeokoa zaidi ya Sh milioni 74 katika maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye miradi ya maendeleo, vyama vya ushirika na mikopo umiza na kuzirejesha kwa wenyewe.

 Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Tabora, Musa Chaulo,  alisema kati ya fedha zilizookolewa Sh 24,640,000 iliyotolewa bila kufuata utaratibu ambazo zimerejeshwa kwa wenyewe.

Alisema taasisi hiyo ilifanya uchunguzi na kubaini uonevu na ukiukwaji mkubwa wa taratibu za ukopeshaji kwani  wakopesha waliwataka wakopaji ambao ni wastaafu riba ya asilimia 500 ndani ya miezi minne.

 Alisema pia kupitia dawati la uzuiaji rushwa, taasisi hiyo imefuatilia mradi wa ujenzi wa majengo na ukarabati  wa miundombiny ya Shule ya Sekondari ya Milambo unaogharimu Sh  522,072,250.

 Alisema walipokea malalamiko 54 ambayo kati yake 29 yalikuwa ya viashiria vya rushwa, watoa taarifa 13 walipewa ushauri kulingana na malamlko yao na 12 yalihamishiwa idara nyingine kwa ufuatiliaji zaidi.

Alisema wakati  wa kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa madiwani, wabunge na Rais utakaofanyika Oktoba mwaka huu, Takukuru  mkoa imeweka mkazo wa kuelimisha jamii  ili kuhakikisha  wanapatikana viongozi wenye maadili.

 Kufuatia hilo Chaulo aliwataka wananchi  na wanasiasa kufuata taratibu na sheria za nchi na kuhakikisha hawajihusishi na vitendo vya rushwa na yeyeto atakaye bainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

 Aliwakumbusha wananchi kutokubali kurubuniwa na wagombea  na kupewa rushwa kwani athari zake ni kubwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles