28.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, January 19, 2022

Msajili aonya vyanzo vya mapato NGO’s kufanywa siri

Mwandishi Wetu

Wamiliki wa Mashirika yasiyo ya serikali (NGO’s), nchini wametakiwa kuhakikisha kuwa taarifa za vyanzo vya fedha za mashirika hayo vinakuwa wazi ili wanajamii waweze kuzifahamu.

Msajili wa Mashirika yasiyo ya kiserikali kutoka Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Neema Mwanga, amesema hayo leo alipofanya kikao na wadau wa mashirika hayo wanaofanya kazi zao katika wilaya zote za Mkoa wa Kilimanjaro.

“Vyanzo vya mapato ya mashirika haya si jambo la siri, tunapoandaa maandiko ya miradi yetu tunatumia taarifa za majina ya wananchi walioathirika katika maeneo husika hivyo mashirika hayo kuficha taarifa za fedha hii si haki,” amesema.

Aidha, amesema kila shirika lisilo la kiserikali sharti liwe na sera ya uendeshaji na Kanuni za maadili pamoja na sera ya kuzuia rushwa mahala pa kazi ili kuhakikisha shirika linalinda maslahi ya taifa na kukuza haki  na utu wa wanajamii wanaonufaika na miradi inayotekelezwa.

Msajili huyo ameelekeza uongozi wa Mashirika hayo kuhakikisha yanafanya tafiti ili kujua na tathmini ya matatizo ya kijamii kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Serikali kabla ya kuomba fedha kutoka kwa wahisani kwa lengo la kutekeleza miradi inayozingatia vipaumbele vya kitaifa na mahitaji ya makundi mbalimbali katika jamii zetu.    

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
175,312FollowersFollow
531,000SubscribersSubscribe

Latest Articles