27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

Msafara wa Jaffo wapata ajali

jafobungeNa Pendo Fundisha, Mbeya

NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jaffo, amenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akisafiria kugongwa upande wa mbele.

Ajali hiyo iliyotokea jana eneo la Katela Kijiji cha Ibura Kata ya Kiwira wilayani Rungwe, ilihusisha gari hilo lenye namba za usajili  DFP 970 ambalo liligongwa na gari lenye namba za usajili T780 AWW Toyota Cresta, likiendeshwa na dereva, Albert Kasilika (42), mkazi wa Uyole jijini hapa.

Akizungumzia ajali hiyo, Jaffo alisema anashukuru Mungu kwa kunusurika katika ajali hiyo kwani ilikuwa mbaya baada ya gari lake kugongwa na kusababisha gurudumu la mbele upande wa kushoto kuchomoka.

“Nikiwa narejea mjini Mbeya, nilikutana na gari Toyota Cresta ikiwa katika mwendokasi na kulivaa gari letu upande wa mbele na kusababisha tairi kuchomoka, lakini gari iliweza kusimama na sisi kuhamia gari nyingine ili kuwahi matibabu,”alisema.

“Mungu ni mkubwa kwani ajali ilikuwa mbaya lakini nimenusurika  na kutoka salama, kubwa zaidi nimefika hapa katika hospitali ya mkoa kuangalia afya yangu ili niendelee na safari ya kuelekea Dodoma,”alisema Jaffo.

Aidha aliongeza kuwa baada ya kufanyiwa vipimo hivyo na wataalamu  wa afya imeonesha kwamba hana tatizo lolote na hivyo aliruhusiwa kuendelea na safari.

Jaffo alikuwa katika ziara ya kikazi wilayani Kyela mkoani Mbeya lakini iliikatisha na kutakiwa kurejea mjini Dodoma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles