30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 30, 2023

Contact us: [email protected]

‘Mrithi’ wa Lissu aanza kwa mkwara bungeni

Anna Potinus

Mbunge wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu amemtaka Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa kumhakikishia uwezekano wa kupata Sh bilioni mbili kwa ajili ya kutengeneza miundombinu itakayowasaidia wananchi wake kupata maji.

Mbunge huyo ameapishwa bungeni leo baada ya kupita bila kupingwa katika Jimbo la singida Mashariki lililokuwa linashikilizwa na Tundu Lissu, ambaye alivuliwa ubunge katika mkutano wa bunge uliopita.

Akiuliza swali la nyongeza katika kipindi cha maswali na majibu, Mtaturu amesema Wilaya ya Ikungi na Jimbo la Singida Mashariki lina matatizo ya maji lakini jitihada zimefanyika kutatua changamoto hizo ambapo kupitia serikali ya awamu ya tano wameshapatiwa Sh bilioni 1.5 kuchimba visima virefu 28.

“Ninamuomba Mheshimiwa Waziri anihakikishie kwamba kupitia tathmini iliyofanywa na ipo wizarani tunahitaji Sh bilioni mbili ili tuweze kutengeneza miundombinu wananchi wa Singida wapate maji maana kuchimba maji na kuyapata ni jambo moja na kutoka maji ni jambo la pili,” amesema.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amemtaka mbunge huyo kukutana naye saa saba mchana wa leo mara baada ya kikao cha bunge kumalizika ili waweze kupanga mkakati wa namna ya kutatua tatizo hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles