24.6 C
Dar es Salaam
Saturday, September 7, 2024

Contact us: [email protected]

MPENZI WA NONDO KUTOA USHAHIDI MAHAKAMANI

Na RAYMOND MINJA-IRINGA


MPENZI anayedaiwa kuwa wa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), ambaye pia ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Abdul Nondo, Veronica Fredy, anatarajiwa kufikishwa mahakamani kutoa ushahidi katika kesi inayomkabili mwanafunzi huyo.

Kesi ya Nondo iliendelea jana katika Mahakama ya Wilaya ya Iringa ambako alifika akiwa na wakili wake Chance Mloga kusikiliza maelezo ya awali kuhusu kesi inayomkabili.

Veronica ni miongoni mwa mashahidi ambao upande wa Jamhuri unakusudia kuwaleta mahakamani.

Mashahidi wengine ni Koplo Salum, Alphonce Mwamule, Koplo Abdulkadir na mfanyakazi kutoka mtandao wa Tigo.

Akisoma maelezo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya  Wilaya ya Iringa, John Mpitanjia, Wakili wa Serikali Abel Mwandalamo, alisema Nondo anakabiliwa na mashtaka mawili ambayo ni kusambaza taarifa za uongo akiwa Ubungo, Dar es Salaam na kutoa taarifa za uongo akiwa mjini Mafinga kwa askari polisi Kituo cha Mafinga wilayani Mufindi.

Hata hivyo, Nondo alikana mashtaka hayo yanayomkabili.

Jamhuri inakusudia kuambatanisha vielelezo vya ushahidi ambavyo ni taarifa za uchunguzi kuhusiana na mawasiliano ya simu, maelezo kutoka Mafinga yakidai Nondo katekwa na simu za mkononi.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 18, mwaka huu itakapokuja kwa hatua ya kuanza kusikilizwa mfululizo.

Machi 21, mwaka huu, Nondo, alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Iringa na kusomewa makosa mawili ya kutoa taarifa za uongo mitandaoni na kudanganya kutekwa.

Nondo alifikishwa mahakamani hapo, baada ya kusafirishwa usiku akitokea Dar es Salaam alikokuwa akishikiliwa na polisi na kusomewa mashtaka hayo na Wakili wa Serikali, Mwandalamo mbele ya Hakimu Mpitanjia.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Wakili wa Nondo, Luoga, alimwomba hakimu kumpatia dhamana mteja wake kwa kuwa makosa hayo yanadhaminika.

Hakimu alisema hawezi kumpa dhamana kwa sababu watekaji bado wako mitaani na wanamshikilia kwa usalama wake na aliahirisha shauri hilo hadi Machi 26, mwaka huu siku ambayo alifanikiwa kutoka kwa dhamana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles