27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

CHANZO CHA MOTO BUNGENI CHATAJWA

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA


CHANZO cha moshi uliotokea juzi usiku ndani ya ukumbi wa Bunge  kimetajwa kuwa ni kifaa cha  ielektroniki cha kuchajia simu ya mkononi (Power Bank) ambacho kilikuwa kikichaji simu mbili kwa wakati mmoja.

Akitoa taarifa   bungeni jana, Naibu Spika wa Bunge,  Dk. Tulia Ackson alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 1:20 usiku wakati kikao cha Bunge kikiendelea.

Alisema ulitokea mlipuko wa kifaa cha  elektroniki cha kuchajia simu ya mkononi uliosababisha harufu kali na kutanda moshi katika ukumbi wa Bunge hasa upande wa kulia wa kiti cha Spika.

“Kwa mujibu wa maelezo ya askari wa Bunge, mlipuko ulitokea kwenye power bank ambayo ilikuwa ikichaji simu mbili kwa wakati mmoja kwenye droo ya meza ya mbunge Richard Mbogo,”alisema.

Alisema   kifaa hicho kiliteketea kwa moto na kilianguka chini na kuunguza zulia na pembeni mwa kiti cha mbunge huyo.

“Katika tukio hilo hakukuwa na majeruhi isipokuwa baadhi ya wabunge walipata mshtuko na baadhi yao walikimbia nje ya ukumbi wa Bunge na waliobaki ndani ya ukumbi walipaliwa na moshi na   kukohoa,” alisema Dk. Tulia

Naibu Spika alisema kutokana na hali hiyo ilimlazimu Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Zungu kuahirisha kikao cha Bunge.

Akiomba mwongozo kwa Spika, Mbunge wa Viti Maalumu, Ruth Mollel (Chadema), alisema haelewi ni kwnini moshi ulitokea ndani na hakuna kifaa cha kiashiria moshi huo.

“Nilitegemea kungekuwa na alarm za kutushtua sisi huku ndani niliona ni jambo very serious lakini sijaona kifaa cha kuashiria na tangu tumekuja humu ndani hatujapewa eneo ambalo tutaweza kukutana kama moto ukitokea na tutokeje,” alisema Mollel.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles