Mpenzi wa Bobbi Kristina afariki dunia

0
858

FLORIDA, MAREKANI 

ALIYEKUWA mpenzi wa marehemu Kristina Bobbi, Nick Gordon, amefariki dunia baada ya kusherehekea siku ya mwaka mpya.

Gordon ambaye amefariki akiwa na miaka 30, anadaiwa kusumbuliwa na tatizo la moyo, lakini amepoteza maisha baada ya kukimbizwa hospitalini kutokana na kutumia dawa za kulevya kupita kiasi.

Gordon alikuwa kwenye uhusiano na marehemu Kristina ambaye ni mtoto wa Bobbi Brown na Whitney Houston, ambapo Kristina alipoteza maisha Julai 26, 2015, kutokana na utumiaji wa dawa za kulevya.

Kifo hicho kilileta utata ambapo Gordon alihusishwa kwamba amesababisha mrembo huyo kutumia dawa za kulevya na sasa anapoteza yeye maisha kwa tuhuma hizo za kutumia dawa za kulevya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here