20.8 C
Dar es Salaam
Saturday, August 20, 2022

Amber Rose aanika mwili wake

LOS ANGELES, MAREKANI 

MWANAMITINDO Amber Rose, kwa mara ya kwanza ameonekana mbele za watu mara baada ya kufanyiwa upasuaji wa kupunguza mwili.

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 36, alifikia maamuzi hayo ya kupunguza mwili mara baada ya kujifungua mtoto wa pili Oktoba mwaka jana na mpenzi wake Alexander Edwards.

Kwa madai yake ni kwamba, baada ya kujifungua hakuonekana kuwa na mwili mwenye mvuto, hivyo aliamua kwenda kufanyiwa upasuaji ili kupunguza nyama mwili na kurudi katika hali yake.

Baada ya kufanikisha upasuaji huo, mrembo huyo kwa mara ya kwanza ameonekana mitaani mara baada ya kusherehekea mwaka mpya. Hata hivyo alitumia kurasa zake za mitandao ya kijamii na kuzianika picha mbalimbali zikimuonesha mrembo huyo akiwa mitaani na muonekano mpya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
199,058FollowersFollow
551,000SubscribersSubscribe

Latest Articles