20.8 C
Dar es Salaam
Saturday, August 20, 2022

Lulu ajuta kumuweka mdogo wake mitandaoni

Na BRIGHITER MASAKI-DAR ES SALAAM

MSANII wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefunguka sababu ya kumtoa mdogo wake Erick kwenye mitandao ya kijamii.

Msanii huyo amedai mdogo wake bado ana umri mdogo, hivyo hawezi kumlazimisha kuja kuwa staa, ila akikua ataamua nini akifanye, lakini kuanza kumuingiza kwenye mitandao kwa sasa ni makosa.

Akizungumza na MTANZANIA jana, amesema alifanya makosa makubwa kumuweka mitandaoni itakuwa kama anamlazimisha kufanya atakalo yeye.

“Nimejifunza kitu katika maisha kuwa, kila mtu na maisha yake hivyo ni vyema nikamuweka nje ya mitandao hadi pale mwenyewe atakapoamua, kwanza ni mwanafunzi yupo darasa la sita anakaribia kumaliza la saba ana miaka 12.

“Nikimuweka sana naweza nikawa naingilia uhuru wake hapo badae anaweza asifurahie kuwa kwenye mitandao, hivyo nimemwondoa ili nisimchagulie maisha ya kuishi na vitu vya kufanya, ila hapo baadae akihitaji basi nitamuunga mkono,”alisema Lulu. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
199,058FollowersFollow
551,000SubscribersSubscribe

Latest Articles