LONDON, UINGEREZA
SERIKALI ya Uingereza inafikiria hatua kadhaa ikiwemo uwezekano wa kuchelewesha uamuzi wake wa kujiondoa kutoka Umoja wa Ulaya (EU) maarufu kama Brexit.
Hilo ni iwapo Bunge la hapa litashindwa kuuidhinisha mpango wa Waziri Mkuu Theresa May kufikia Machi 12.
Zikiwa zimebakia siku 32 kufikia tarehe ya nchi hiyo kuondoka EU, uamuzi wa May wa kuisogeza tarehe ya kupiga kura juu ya hatma ya mpango wake imesababisha mvutano.
Bunge limegawanyika kuhusu namna nchi hii inavyotakiwa kujiondoa EU au hata pengine iwapo kuna umuhimu wa kuondoka katika umoja huo.
Kabla ya mchakato wa kuupigia kura mpango wa May kesho, wabunge wamekuwa wakiimarisha njia za kujaribu kumzuia kuiondoa Uingereza kutoka Umoja wa Ulaya bila ya makubaliano