28.1 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

Trump, Kim Jong Un wajiandaa kukutana Vietnam

HANOI, VIETNAM         

RAIS Donald Trump wa Marekani amesema ataendelea kuwa na furaha kad8iri Korea Kaskazini inavyoendelea kuacha kufanya majaribio ya makombora yake.

Aidha alisema hana pupa ya kufikia makubaliano ya nyuklia na kiongozi wa nchi hiyo, Kim Jong Un.

Alisema hayo wakati viongozi hao wakitarajia kukutana kwa mkutano wao wa pili wa kilele kesho au keshokutwa mjini hapa.

Mkutano huo unakuja miezi minne baada ya mkutano wao wa kihistoria wa kwanza uliofanyika Singapore.

Katika mkutano wa Singapore, waliahidi kushirikiana kuelekea hatua ya kuondoa kabisa silaha za nyuklia katika Rasi ya Korea, lakini makubaliano yao yasiyo rasmi yamekuwa na mafanikio madogo.

Nchini Marekani, maseneta wa chama cha Democrats pamoja na maofisa wa usalama wamemuonya Trump dhidi ya kufikia makubaliano ambayo hayatakuwa na uwezo wa kuizuia nia ya Korea Kaskazini ya kutengeneza silaha za nyuklia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles