WASHINGTON, MAREKANI
NUSU ya wataalamu wote wa uchumi nchini hapa wanasema wanadhani uchumi wa taifa hilo utatumbukia katika mporomoko kufikia mwishoni mwa mwaka ujao.
Baadhi ya wanauchumi wanakadiria kwamba mtikisiko mkubwa wa kiuchumi utaanzia mwishoni mwa mwaka 2021.
Utafiti huo umetokana na uchunguzi uliofanyika karibuni na Chama cha Taifa cha Wanauchumi na Wafanyabiashara nchini Marekani (NABE).
Asilimia 10 tu ya wanauchumi hao wamekadiria kuwa mtikisiko wa uchumi utaanza katika kipindi hiki cha mwanzo wa mwaka huu.
Asilimia 11 ya wanauchumi wanatarajia kwamba mporomoko wa kiuchumi utaepukika mwaka 2021.
NABE ndiyo wenye dhamana ya kuhakiki usimamizi wa viwango vya riba vya hazina kuu ya Marekani.