27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mpango wa kumwondoa Trump washindikana tena bungeni

WASHINGTON,MAREKANI

MPANGO wa kumwondoa Rais wa Marekani, Donald Trump kwa kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye ndani ya Bunge, umekwama.

Kusudi hilo ambalo liliwasilishwa kwenye Baraza la Wawakilishi na Mwakilishi wa Texas kupitia chama cha Democrat, Al Green lilitokana na mashambulizi ya maneno yenye ubaguzi wa rangi yaliyotolewa na Trump dhidi ya wabunge wanawake wa chama cha Democrat mapema wiki hii.

Hata hivyo mpango huo ulikwama kupata sapoti ya kutosha, baada ya wawakilishi wa Democratic kuzidiwa kwa wingi wa kura.

Taratibu za kumwondoa rais wa Marekani madarakani kwa kawaida zinaanzia ndani ya Baraza la Wawakilishi ambako mjumbe yeyote anaweza kupeleka hoja hiyo iwapo anamtuhumu rais kwa uhaini, rushwa na uhalifu wowote wa juu au ukosefu wa nidhamu.

Ili hatua hiyo ya kwanza ipite kabla haijafika Mahakama ya juu inabidi wawakilishi wapige kura na kupitisha azimio hilo kwa  asilimia 51 jambo ambalo limeshindikana kwa mara ya tatu sasa.

Trump mwenyewe alielezea hatua hiyo kama ni ya kijinga.

“Hili halitakiwi kutokea tena kwa Rais yeyote wa Marekani!” aliandika Trump kupitia akaunt yake ya Twitter.

Baadae akiwa katika mkutano huko North Carolina, Trump aliendeleza mashambulizi dhidi ya wabunge hao wanawake wa chama cha Democrat wasio wazungu ambao ni Alexandria Ocasio-Cortez, Ilhan Omar, Ayanna Pressley na Rashida Tlaib, ambao sasa wamepachikwa jina la “the squad”.

Huku akifurahia pamoja na umati wa wafuasi wake, Trump aliwashutumu tena wanawake hao kwamba wanaichukia Marekani.

Kauli hiyo iliwafanya wafuasi wake waanze kuimba “mrudishe! mrudishe!”- “mfunge “.

Awali kabla ya hatua ya sasa mapema wiki hii Trump alidai wanawake hao wamewasili kutoka mataifa ambayo serikali zake ni majanga matupu, na  kupendekeza warudi walikotoka.

Alisema Spika Nancy Pelosi atafurahi  kushughulikia haraka mipango ya safari ya bure ya kuwarudisha kwao.

Kauli hiyo ya Trump ilikuja baada ya Pelosi kukabiliana kwa maneno na kundi la wabunge wasio watu weupe wa mrengo wa kushoto wa chama cha Democrat.

Kati ya wabunge hao wanne, watatu – Alexandria Ocasio-Cortez, Rashida Tlaib na Ayanna Pressley – walizaliwa na kulelewa Marekani, huku wanne, Ilhan Omar, alihamia Marekani alipokuwa mtoto.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles