24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 21, 2023

Contact us: [email protected]

Aliyekamatwa na samaki wa sumu apigwa faini

Gurian Adolf-Nkasi

MAMLAKA ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) wilayani Nkasi mkoani Rukwa, imesema haitamfikisha mahakamani mfanyabishara wa samaki, Dernest Batupu aliyekamatwa kwa kosa la kuhifadhi samaki ili wasiharibike kwa kutumia sumu aina ya Dip inayotumia kuuia kupe.

Akizungumza na MTANZANIA mjini hapa juzi, Mratibu wa TFDA,Consolata Mwingila alisema kutokana na mtuhumiwa kukiri kosa na kuadhibiwa kulipa faini ya Sh 1000,000, hakuna sababu kisheria ya kumfikisha mahakamani kwa kuwa tayari ameadhibiwa.

Alisema kwa mujibu wa taratibu za kisheria, mtuhumiwa alipaswa kufikishwa mahakamani bila kutozwa faini.

Alisema kama atafikishwa mahakamani,basi awe ametenda kosa jingine.

”Haiwezekani mtu mmoja akapewa adhabu mara mbili kwa kosa moja,alikiri na kulipa faini ya shilingi 1000,000, hakuna sababu ya kumfikisha mahakamani,” alisema.

Alisema iwapo akibainika kuendelea na mchezo huo kamwe mamlaka haitamfumbia macho, atakamatwa upya na kufikishwa mahakamani kwani lengo ni kukomesha tabia hiyo.

Alisema mfanyabiashara huyo, alikamatwa na samaki hao wakavu waliokuwa wamehifadhiwa kwa kutumia sumu aina ya Dip ili wasiharibike.

Aliwaonya wafanyabiashara wa samaki hao wanaowasafirisha ndani na nje ya nchi kwa lengo la kutafuta soko pamoja na bidhaa nyingine kutotumia kemikali zozote.

Alisema kemikali hizo, zina madhara makubwa kwa binadamu.

Hivi karibuni TFDA kwa kushirikiana na viongozi wa Wilaya ya Nkasi, iliteketeza tani mbili za samaki wakavu waliokuwa wamehifadhiwa kwa kutumia sumu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
210,784FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles