25.5 C
Dar es Salaam
Thursday, September 28, 2023

Contact us: [email protected]

MOURINHO: POGBA NI SAWA NA MESSI, NEYMAR

WASHINGTON DC, MAREKANIKOCHA wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho, ameweka wazi kuwa, uwezo wa kiungo wake, Paul Pogba, unafaa kufananishwa na mastaa wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi na Neymar.

Kocha huyo amedai Pogba alionesha kiwango cha hali ya juu kwenye mchezo wa jana dhidi ya Barcelona, japokuwa timu yake ilipokea kichapo cha bao 1-0 kwenye mchezo huo wa kirafiki wa kujiandaa na msimu mpya.

Manchester United jumla imecheza michezo mitano ya kirafiki katika kipindi hiki cha majira ya joto na kujikuta ikishinda minne na kupoteza mchezo huo mmoja dhidi ya Barcelona, lakini Mourinho amedai Pogba alionesha kiwango cha hali ya juu katika eneo lake la katikati.

“Messi na Neymar, hawa ni wachezaji wa aina yake, hivyo kuna Messi mmoja na Neymar mmoja duniani, hata hivyo, wachezaji wengine kama vile Suarez, Iniesta, Pique, Ronaldo, Bale, Modric, Toni Kroos wako peke yao.

“Lakini naweza kusema mchezaji wangu, Paul Pogba, katika mchezo wa leo (jana), ameonesha kuwa uwezo wake ni mkubwa na anastahili kuwa kwenye orodha ya wachezaji bora kama Messi na Neymar.

“Hao ni wachezaji wa kipekee duniani na hauwezi kuwafananisha na wengine, unaweza kujaribu kuwafananisha, lakini bado watakuwa tofauti. Ukiwa na wachezaji kama hao kwenye kikosi ni rahisi kupata mataji,” alisema Mourinho

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,750FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles