Mourinho aitupia lawama safu ya ulinzi

0
637

Manchester United v Chelsea - Premier LeagueLONDON, ENGLAND

KOCHA wa Chelsea, Jose Mourinho, ametupia lawama safu ya ulinzi ya klabu hiyo baada ya kupokea kichapo cha
mabao 2-1 dhidi ya Porto.

Kocha huyo amesema mpaka sasa hajui ubora wa kikosi chake kwa kuwa kimepoteza michezo mingi ya Ligi Kuu nchini England.

“Kuna tatizo kwa upande wa safu ya ulinzi na ndio maana tunapoteza baadhi ya michezo, hii inatokana na kukosa mawasiliano lakini ninaamini nina mabeki wazuri ambao wana uwezo mkubwa na wala sina wasi wasi.

“Matatizo yanakuja pale unapopoteza mchezo, ila ninaimani na kikosi changu na tutafanya vizuri katika michezo ijayo,” alisema Mourinho.

Hata hivyo, kocha huyo amejikingia kifua kwa maamuzi aliyoyafanya katika mchezo wa juzi dhidi ya Porto kwa kuwaacha washambuliaji wake Radamel Falcao na Loic Remy.

“Nimefanya maamuzi sahihi ya kuwaacha washambuliaji wangu Radamel Falcao na Loic Remy, wala si adhabu, ninaamini kikosi kina wachezaji wazuri na ndio maana nilifanya hivyo.

“Kutokana na matokeo haya najua wapi kuna tatizo, hivyo katika michezo ijayo nitahakikisha naweka sawa,” aliongeza Mourinho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here