26.7 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Wenger ashindwa kueleza sababu za kumuacha Cech

wengerLONDON, ENGLAND

BAADA ya Arsenal kupokea kichapo cha mabao 3-2 katika michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya dhidi ya
Olympiacos, kocha wa klabu hiyo Arsene Wenger ameshinda kueleza sababu za kumueka benchi kipa namba moja Petr Cech na kumpa nafasi David Ospina.

Huo ulikuwa ni mchezo wa pili Arsenal inapoteza katika michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa, ambapo katika mchezo
wa awali klabu hiyo ilikutana na Dinamo Zagreb na kuchezea kichapo cha mabao 2-1.

Hata hivyo, baada ya kumalizika kwa mchezo huo wa juzi, Wenger aliulizwa na waandishi wa habari sababu za kumuacha benchi mlinda mlango wake Cech na kumpaka nafasi Ospina lakini alishindwa kueleza sababu.

“Siwezi kueleza sababu ya kila jambo ambalo nitalifanya, lakini kila mtu anajua uwezo wa Ospina na Cech wote ni walinda lango wazuri hivyo nilikuwa na uamuzi wa kumpa nafasi mchezaji yeyote.

“Ospina alionesha kiwango cha hali ya juu katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Tottenham wiki iliyopita, hivyo naweza kusema kati ya walinda mlango hao hakuna ambaye ameonekana kucheza chini ya kiwango.

“Ninaamini nimefanya maamuzi sahihi na maswali mengi yanajitokeza kutokana na kupoteza mchezo huu, lakini sina muda wa kulijadili suala hilo,” alisema Wenger.

Kutokana na matokeo hayo, Arsenal kwa sasa inashika nafasi ya mwisho katika kundi F huku ikiwa haina pointi baada ya kucheza michezo miwili huku wakitarajia kucheza na wababe wa kundi hilo Bayern Munich ambao mpaka sasa wameshinda michezo yao yote ya Ligi Kuu nchini Ujerumani na Ligi ya Mabingwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles