25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, December 9, 2023

Contact us: [email protected]

Kisamke, VanGaalkustaafusoka

Van GaalMANCHESTER, ENGLAND

KOCHA wa Manchester United, Van Gaal, amesema mipango yake ya kustaafu soka baada ya kumaliza mkataba katika klabu hiyo bado ipo pale pale kwa kuwa alimuahidi mke wake.

Van Gaal amesisitiza kuwa hawezi kumuangusha mke wake Truus kwamba akimaliza mkataba wake mwaka 2017 ataachana na soka ili aweze kutulia na familia yake, hata hivyo kocha huyo amesema hana uhakika kama itawezekana kutokana na jinsi anavyopenda mpira.

“Ninaamini nitaondoka baada ya kumaliza mkataba wangu, lakini sidhani kama nitakuwa sahihi kwa maamuzi hayo huwezi jua, ila nakumbuka nilimuahidi mke wangu kwamba nikimaliza mkataba wangu na klabu ya United nitastaafu ili niweze kuwa na familia yangu.

“Itakuwa ngumu kuvunja ahadi hiyo kwa kuwa nilisema hivyo huku nikiwa na miaka 55 na ikifika mwaka 2017 nitakuwa nimefikisha miaka 65 na nikishindwa kufanya hivyo nitakuwa nimemkosea mke wangu,” alisema Van Gaal.

Kwa sasa klabu hiyo inafanya vizuri katika michuano ya Ligi Kuu nchini England ambapo inaongeza katika msimamo wa ligi huku ikiwa na pointi 16 baada ya kucheza michezo saba.

Timu hiyo ina nafasi kubwa ya kufanya vizuri msimu huu katika michuano mbalimbali, kutokana na ubora wa kikosi chake baada ya kocha huyo kufanya usajili mkubwa katika kipindi cha majira ya joto

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles