27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, December 7, 2023

Contact us: [email protected]

Casillasafurahiakuifunga Chelsea, siMourinho

casillasRIBEIRA, PORTO

MLINDA mlango wa klabu ya Porto, Iker Casillas, amesema amekuwa na furaha kubwa ya kuifunga Chelsea na si kumfunga kocha wake wa zamani Jose Mourinho.

Awali wawili hao waliwahi kufanya kazi pamoja katika klabu ya Real Madrid, lakini Casillas anaamini kuwa kiwango
chake kilishuka kutokana na tabia ya kocha huyo kumuweka benchi katika michezo mbalimbali.

Hata hivyo, Casilas mwanzoni mwa Septemba alisema Mourinho amemfanya thamani yake ishuke katika soka hivyo hana uhusiano mzuri na kocha huyo, lakini katika mchezo wa juzi wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya ulikuwa wa kwanza kuwakutanisha wawili hao.

Katika mchezo huo wa juzi Chelsea ilijikuta ikiambulia kichapo cha mabao 2-1 na kumfanya mlinda mlango huyo kuwa na furaha kubwa kutokana na ushindi huo.

“Sina furaha kwa sababu nimemfunga kocha wangu wa zamani Jose Mourinho, lakini nina furaha kubwa kwa sababu
nimeisaidia timu yangu kuipa ushindi.

“Sina tatizo na Mourinho na hata kabla ya mchezo niliweza kusalimiana na kocha huyo kwa kushikana mikono, siwezi kukumbuka ya zamani ambayo alinifanyia nikiwa Madrid, kwa sasa ni kuangalia yajayo,” alisema
Casillas.

Mchezo huo ilipigwa katika Uwanja wa Estadio do Dragao na kuwafanya Porto wafanikiwe kushika nafasi ya pili katika kundi G.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles