Mourinho ageuka mbogo Man Utd

0
948

jose-mourinhoMANCHESTER, England

KOCHA wa Manchester United, Jose Mourinho, jana aliwatuhumu wachezaji wake kwa kushindwa kujifunza makosa waliyofanya katika mchezo dhidi ya Manchester  City.

Kocha huyo aliyasema hayo baada ya kushuhudia  kikosi chake juzi  kikipoteza  mchezo mwingine wa tatu kwa  kuambulia kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Watford.

Mourinho alianza kwa kumlaumu beki wa kushoto wa timu hiyo, Luke Shaw, akidai kuwa alifanya kosa linalofanana katika mchezo dhidi ya Manchester City.

Nyota huyo alisababisha penalti na kusababisha kufungwa bao la tatu baada ya kumfanyia madhambi mchezaji wa timu pinzani, Camilo Zuniga.

“Baadhi ya wachezaji wangu walikuwa katika presha wakijua wana majukumu zaidi ya wengine hivyo huenda  ikawa sababu ya kupoteza michezo hiyo mfululizo.

“Tulianza msimu katika hali ya mafanikio na  nilijua  tayari timu yangu ipo katika mapambano, nilishtuka nilipoanza kupoteza,” alisema Mourinho.

Mourinho anaongezea kuwa hakujua  kwamba kikosi chake hakikuwa  tayari wala  kuwapo na wachezaji ambao si sahihi  na muda wowote wanaweza kufanya makosa.

Kocha huyo hadi sasa amepoteza michezo mitatu katika msimu huu ikiwa ni mara ya kwanza tangu afanye hivyo mwaka 2002 akiwa  kocha wa  timu ya FC Porto.

United wameshinda kombe la Community Shield na michezo mitatu ya Ligi Kuu England ikiwa chini ya kocha huyo ambaye ni mbadala wa aliyekocha wa timu hiyo, Louis van Gaal.

Lakini inafahamika baada ya kufungwa dhidi ya Manchester City wiki iliyopita ilichangia kupoteza pia dhidi ya Feyenoord katika mchezo wa Europa uliochezwa wiki iliyopita.

Baada ya kupoteza dhidi ya Watford, timu hiyo kwa sasa ipo nafasi ya saba katika msimamo wa Ligi Kuu England.

Mourinho anaamini kikosi chake kimekuwa hakifanyi vizuri kutokana na makosa ya waamuzi hasa katika mchezo dhidi ya Watford.

Kocha huyo pia analalamika katika mchezo dhidi ya Manchester City    alitakiwa kupata penalti.

“Waamuzi wanafanya makosa mengi uwanjani hata hivyo siwezi kuwadhibiti na hakuna ninachoweza kufanya katika hilo.

“Tuliadhibiwa kwa makosa ambayo  hayakuwa sahihi kwetu lakini siwezi kufanya jambo lolote,” alisema Mourinho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here