25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Serengeti Boys itafuzu kwenda Madagascar

shimeTHERESIA GASPER NA WINFRIDA NGONYANI-DAR ES SALAAM

KOCHA mkuu wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Boys’, Bakari Shime, amesema kikosi chake kitafanya vema kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Congo Brazzaville, licha ya kucheza ugenini na kufanikiwa kufuzu fainali za Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 zitakazofanyika mwakani nchini Madagascar.

Juzi Serengeti Boys walifanikiwa kuwafunga Congo Brazzaville mabao 3-2, katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Shime alisema kikosi chake hakiangalii ugenini ila kinapambana kwenye uwanja wowote na kufanikiwa kupata ushindi.

“Vijana wangu walijitahidi na kupata mabao ya mapema, lakini wapinzani wetu walitumia vizuri makosa waliyoyafanya vijana na kuruhusu kufunga mawili,” alisema.

Alisema kukosekana kwa wachezaji Dickson ambaye ana kadi ya njano na Ally Nyanze mwenye nyekundu, kulisababisha kupungua kwa safu ya ulinzi katika eneo la kati.

Shime aliwataka Watanzania kuwa na moyo na kuendelea kutoa sapoti kwa vijana hao, ili wafanikiwe kufanya vema kwenye mchezo wa marudiano.

Katika hatua nyingine, Serengeti Boys itaondoka nchini keshokutwa tayari kwenda Madagascar, kwa ajili ya kuweka kambi ya muda mfupi.

Serengeti Boys inakwenda Madagascar ambako fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana zitafanyika hapo mwakani na itajichimbia  kabla ya kuelekea kwenye mechi ya marudiano dhidi ya Congo Brazzaville itakayochezwa nchini humo, Oktoba 2 mwaka huu.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas, aliliambia MTANZANIA kuwa Serengeti itakaa nchini humo kwa siku kumi.

“Timu itaondoka Alhamisi wiki hii na itaenda kuweka kambi nje ya nchi lakini hadi sasa nchi ambayo tunaifikiria ni Madagascar, itakaa kwa siku kumi na baadaye itaenda nchini Congo,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,430FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles