27.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 8, 2024

Contact us: [email protected]

Morsi azikwa, familia, jumuiya ya kimataifa yataka uchunguzi

-Cairo

RAIS wa zamani wa Misri, Mohamed Morsi, amezikwa saa chache baada ya kufariki dunia akiwa mahakamani juzi.

Wakili wake ameliambia Shirika la Habari la Ufaransa (AFP), kuwa Morsi alizikwa jana asubuhi mashariki mwa Jiji la Cairo tukio ambalo lilishuhudiwa pia na familia yake.

Morsi (67), alikuwa kizuizini tangu alipoondolewa madarakani mwaka 2013 ambapo kwa sasa makundi ya watetezi wa haki za binaadamu yalikosoa mazingira ambayo Morsi aliwekwa, yametoa wito wa kufanyika uchunguzi wa kifo chake.

Morsi alikua kiongozi wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia mwaka 2012, aliondolewa na kushikiliwa baada ya mapinduzi ya kijeshi mwaka mmoja baadae baada ya kufanyika maandamano makubwa kupinga utawala wake.

Familia yake na wanaharakati wamezungumzia kufo chake na muda ambao aliwekwa katika seli ya peke yake, akizuiwa kutembelewa na wanasheria na familia yake.

Mtoto wa marehemu, Abdullah Mohamed Morsi, juzi alisema mamlaka za Misri ziliikatalia familia kufanya maziko katika mji yalipo makazi yake.

Baada ya kuondolewa madarakani, mamlaka zilipambana na wafuasi wake na wapinzani wengine na kukamata maelfu ya watu.

Muslima Brotherhood na Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, mshirika wa karibu wa Morsi ni miongoni mwa walioshutumu utawala wa Misri kuhusu kifo cha Morsi.

Kulitokea nini mahakamani

Maofisa wanasema aliomba kuzungumza mahakamanu na kuongea kwa dakika tano kutoka kwenye kizimba kilichokua na kioo ambacho alikuwamo na washtakiwa wengine.

Dakika chache baadae alizimia wakati wa mapumziko mahakamani hapo.

”Alipelekwa hospitali ambapo alithibitishwa kupoteza maisha,”taarifa ya mwendesha mashtaka ilieleza.

Maofisa walisema kuwa hakuna majeraha yeyote ambayo yalionekana mwili mwake.

Televisheni ya Taifa ilieleza awali kuwa chanzo cha kifo chake ni mshtuko wa moyo.

Mosri tayari alikuwa anatumikia kifungo kutokana na mashtaka matatu yaliyokuwa yakimkabili. Awali alihukumiwa adhabu ya kifo ambayo baadae ilitenguliwa.

Shirika la Amnesty International limetaka uchunguzi ufanyike kuhusu kifo chake.

Limesema Morsi alikua akiruhusiwa kutembelewa mara tatu tu kwa miaka sita na hakuruhusiwa kuonana na mawakili wake wala daktari.

Mbunge wa Uingereza, Crispin Blunt, aliyeongoza jopo la wanasiasa na kutoa tahadhari kuhusu kutendewa kwa Morsi mwaka 2018, ametaka ufanyike ”uchunguzi huru kimataifa”

Morsi ni nani?

Morsi alizaliwa katika Kijiji cha El-Awwadh katika jimbo lililopo kwenye delta za Mto Nile la Sharqiya mwaka 1951.

Alisomea Uhandisi katika chuo Kikuu cha Cairo katika miaka ya 70 kabla ya kuhamia nchini Marekani ambapo alitunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Uhandisi.

Morsi aliweka rekodi ya kuwa kiongozi wa kwanza kuchaguliwa katika uchaguzi mwaka 2012, akiwa kiongozi mwandamizi wa kundi la kiislamu la Muslim Brotherhood ambalo limepigwa marufuku kwa sasa nchini humo.

Hata hivyo utawala wake ulikumbwa na wimbi la maandamano ya wanaharakati ambao walimshutumu yeye na kundi la Muslim Brotherhood kujilimbikizia madaraka.

Baada ya maandamano kuwa makubwa na wafuasi wa Morsi kushambulia wapinzani wake, jeshi likiwa chini ya Rais wa sasa, Abdel Fattah el-Sisi, liliendesha mapinduzi na kumng’oa Morsi madarakani, Juni 2013.

Jeshi liliendelea kupambana na wafuasi wa Morsi baada ya mapinduzi na zaidi ya wafuasi wake 1,000 waliuawa Agosti 2013.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles