29.4 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

Trump, Putin kufanya mazungumzo

Moscow 

IKULU ya Urusi imearifu kwamba Rais Vladmir Putin na mwenzake wa Marekani, Donald Trump, huenda wakakutana kwa muda mfupi katika mkutano wa kundi la nchi tajiri kiviwanda na zile zinazoinukia kiuchumi la G20 utakaofanyika Japan wiki ijayo.

Msemaji wa Putin, Dmitry Peskov, aliwaambia waandishi wa habari kuwa viongozi hao hawatokuwa na mkutano kamili watakapokutana kwenye mkutano huo wa kilele utakaofanyika mjini Osaka kuanzia Juni 28.

Wiki iliyopita Trump alisema atakutana na Putin pembezoni mwa mkutano huo wa Japan lakini alitaka mkutano huo uhudhuriwe pia na watu wengine kwasababu waandishi wa habari hawana wanachokiamini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles