24 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Mongela: Ni bora kumpigia kura mgombea mwanamume

Ramadhan Hassan – Dodoma

BALOZI  Getruda Mongela, amesema ni heri kumpigia kura mgombea mwanaume katika chaguzi mbalimbali kuliko mwanamke anayeona aibu kuzungumzia matatizo na  maendeleo ya wanawake.

Akizungumza jana katika mkutano uliowakutanisha viongozi wanawake nchini, Balozi Mongela alisema siku ambayo Bunge litafikia kuwa asilimia 50 ya wanawake hatajali mbunge ametoka chama gani.

Alisema isipokuwa atajali kama mambo wanayozungumza wanawake nchini anayajua na kuyapenda.

“Kama mwanamke yoyote anaingia bungeni akiwa kama ameenda katika maonyesho ya Sabasaba ni heri nimpigie (kura) mwanaume. Ni hasara kuwa na wanawake viongozi wanaoona aibu kuzungumza maendeleo ya wanawake,” alisema.

Alihoji kama wabunge wanawake wanaangalia bajeti ya Serikali ambayo nyingi inaingia katika ujenzi na ni ngapi ambazo zinawafikia wanawake kule vijijini.

“Tunafanya nini fedha nyingi ambazo na wakinamama wamezihangaikia zinafika hadi mikononi mwa wanawake. Na tunatafuta wapi hizo rasilimali?”alihoji.

Naye, Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini, Hodan Addou alisema kuwa leo Mtandao wa Wanawake Afrika tawi la Tanzania,  utazinduliwa ukiwa na malengo mbalimbali ikiwemo kuwahimiza wanawake na viongozi wanawake kutimiza majukumu yao katika kuibadilisha Afrika.

Alitaja lingine ni kuhamasisha majadiliao ili kupitia viongozi  kuhusu mambo yanayowasumbua wanawake barani Afrika.

“Kuwasaidia wanawake viongozi wa kisiasa na wa bara, taifa na ngazi za chini kuweza kutimiza malengo yao ya uongozi,” alisema.

Kwa upande wake Mwenyekiti Mweza wa Mtandao huo, Mary Rusimbi alisema uwepo wao katika mkutano huo unalenga katika kujiangalia, kujitathimini, kujitafakari uongozi wa mwanamke uliko.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles