30 C
Dar es Salaam
Saturday, December 4, 2021

Rais wa zamani wa Misri afariki dunia

Mwandishi wetu

Rais wa zamani wa Misri, Hosni Mubarak amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 91 wakati akipatiwa matibabu katika hospitali moja ya jeshi jijini Cairo baada ya kufanyiwa upasuaji mwishoni mwa mwezi uliopita.

Mtoto wake wa kiume wa Mubarak, Omar Alaa amesema siku ya Jumamosi baba yake alikuwa katika hali mbaya sana, kifo chake kimethibitishwa na Televisheni ya taifa ya nchini humo.

Mubarak alikaa madarakani tangu mwaka 1981 – 2011 kabla ya kung’atuliwa na jeshi baada ya kukutwa na hatia ya kula njama katika mauaji ya waandamanaji wakati wa mapinduzi na kuhukumiwa kwenda jela.

Hata hivyo, hatia hiyo iliondolewa na akaachiwa huru Machi 2017.

Lakini licha ya mabilioni ya dola ya misaada ya kijeshi ambayo Misri ilipokea wakati alipokuwa madarakani, ukosefu wa ajira, ufukara, na ufisadi uliendelea kuimarika nchini humo.

Mnamo Januari 2011, ulizuka mgogoro mkumbwa baada ya wananchi wa Tuinisia kuandamana na kusaidia kupinduliwa kwa rais wa taifa hilo hali iliyopelekea Mubarak kulazimishwa kujiuzulu siku 18 baadaye.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,968FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles