23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

MOI yafanya upasuaji wa fuvu kwa darubini

MVERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM

MADAKTARI Bingwa wa Upasuaji ubongo wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), wamefanikiwa kufanya upasuaji mgumu wa kuondoa uvimbe uliokuwa chini ya fuvu la kichwa kwa kutumia darubini ya kisasa.

Akizungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo jana Daktari Bingwa wa Upasuaji Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu MOI, Nicephorus Rutabasibwa alisema upasuaji huo ni mgumu na huchukua muda mrefu kukamilika.

“Tumefanikiwa kufanya upasuaji huo kwa kushirikiana na mabingwa wenzao kutoka  Hospitali ya Kimataifa ya Chuo Kikuu cha Peking cha nchini China.

“Tumepokea jopo la mabingwa watatu, ushirikiano wetu ni wenye manufaa makubwa kwani huduma za MOI zitaendelea kuwa bora na watanzania wataendelea kupata huduma hizo hapa nchini billa ya kwenda nje ya nchi.

“huu ni muendelezo wa ushirikiano tulioingia na wenzetu hawa wa Peking mwaka jana, tunaamini tutabadilishana uzoefu na wenzetu hawa ambao wamepiga hatua kubwa kwenye teknolojia ya matibabu, kupitaia ushirikiano huu mbinu tunazopata zitatusaidia kuendelea kutoa tiba bora na kwa wakati kwa wagonjwa wetu” alisema.

Alisema ujio huu wa wataalamu kutoka peking umelenga kuweka mazingira bora ya ushirikiano na MOI ili watakapo kuja tena wajue ni maeneo gani yanahitaji kuwa kipaumbele kwenye ushirikiano.

Kiongozi wa jopo la madaktari bingwa kutoka Peking, Profesa Yuani Zhao, alisema ushirikiano kati ya MOI na Peking utakuwa wenye mafanikio makubwa na utawanufaisha wagonjwa pamoja na madaktari vijana ambao watapata fursa ya kusoma kwenye chuo chao.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,549FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles