23.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 3, 2023

Contact us: [email protected]

Mlinda mlango Newcastle afariki dunia

Pavel SrnicekPRAGUE, JAMHURI YA CZECH

MLINDA mlango wa zamani wa timu ya Newcastle, Pavel Srnicek, amefariki dunia kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa moyo.

Nyota huyo ambaye amefariki huku akiwa na umri wa miaka 47, aliugua ugonjwa huo kwa siku tisa na kupoteza maisha yake.

Srnicek, enzi za uhai wake aliwahi kuchezea klabu ya Sheffield Wednesday, Portsmouth West Ham na Newcastle, wakati huo akiitumikia timu ya Taifa ya Jamhuri ya Czech, ambayo aliitumikia kwa michezo 49.

Mchezaji huyo alianza kuitumikia klabu ya Newcastle jumla ya michezo 190 kuanzia miaka ya 1990 hadi 2007 kabla ya kujiunga na klabu ya AC sparta prague

Wakala wa mchezaji huyo, Steve Wraith, amesema baada ya marehemu kufanyiwa uchunguzi wa sehemu yake ya ubongo mwanzoni mwa wiki hii, ilionekana kuwa una matatizo la kudumu hivyo hasingeweza kuendelea kuishi.

“Srnicek alifariki juzi mchana Desemba 29, mbele ya familia yake, hili ni pigo kubwa kwa familia hiyo pamoja na klabu ambazo aliwahi kuchezea na wapenzi wa soka kwa ujumla,” alisema Wraith.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles