Refarii ‘mpenzi wa jinsia moja’ kulipwa fidia

0
764

Halil DincdagANKARA, UTURUKI

MWAMUZI mmoja nchini Uturuki, Halil Dincdag, aliyefukuzwa kazi kwa tuhuma ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja, ameshinda kesi dhidi ya shirikisho la soka la nchini humo.

Mahakama nchini Uturuki imeamuru shirikisho hilo kumlipa fidia mwamuzi huyo kiasi cha dola za Marekani 8,000 kutokana na kushinda kesi hiyo.

Dincdag amefurahia ushindi huo na kusema kuwa ni ushindi kwa watu wanaobaguliwa kijinsia hasa katika michezo nchini Uturuki.

“Sio ushindi wangu peke yangu ila ni kwa ajili ya wale wote ambao wanabaguliwa kijinsia hasa katika michezo mbalimbali, hivyo ni ushindi wa watu wote,” alisema Dincdag.

Mwamuzi huyo sasa amesema atarejea mahakamani kulitaka shirikisho hilo la soka kumrejeshea leseni yake ili aweze kuendelea na kazi.

Shirikisho hilo la soka limesema kuwa Dincdag alifukuzwa kazi kwa sababu ya uchunguzi wa kitaalamu na sio kashfa hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here