30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 1, 2023

Contact us: [email protected]

Van Gaal kupewa ukurugenzi Uholanzi

Van GaalAMSTERDAM, UHOLANZI

TIMU ya Taifa ya Uholanzi, ipo tayari kumpa nafasi kocha wa zamani wa timu hiyo, Louis van Gaal, kuwa Mkurugenzi wa ufundi kama atafukuzwa na uongozi wa klabu ya Manchester United.

Uongozi wa klabu ya Manchester United ulimpa kocha huyo michezo miwili ili kuweza kulinda kiwango chake, lakini michezo hiyo bado hakufanya vizuri ambapo mchezo wa kwanza alifungwa mabao 2-0 dhidi ya Soke City wakati mchezo wa pili akitoka suluhu dhidi ya Chelsea.

Kwa sasa kocha huyo anangoja maamuzi ya uongozi wa klabu hiyo kama utamfukuza ama kuendelea naye japokuwa mkataba wake unatarajia kumalizika mwaka 2017.

Chama cha soka nchini Uholanzi, kimesema kipo tayari kumchukua kocha huyo kuja kuwa Mkurugenzi wa ufundi wa timu ya Taifa endapo United itaamua kuachana nayo.

“Sijui nini kitatokea baada ya kumalizana na Manchester United, lakini bado sijafanya naye mazungumzo binafsi ila jambo hilo linawezekana kwa kuwa tunahitaji mchango wake kwa kuutambua umuhimu wake.

“Atatufaa kwenye suala la ufundi kama tutakubaliana naye, ila kwa sasa tunaheshimu uwepo wake katika klabu ya Manchester United,” alisema kocha wa Uholanzi, Danny Blind.

Hata hivyo, kocha huyo aliwahi kusema kuwa mara baada ya kumalizana na uongozi wa klabu hiyo atastaafu soka kwa kuwa alimwahidi mke wake kuwa anahitaji kupumzika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,396FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles