23.7 C
Dar es Salaam
Thursday, September 28, 2023

Contact us: [email protected]

Mkurugenzi amtumbua mtuhumishi wa halmashauri

Janeth Mayanja
Janeth Mayanja

Na IMMACULATE MAKILIKA, MAELEZO

MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Bunda, mkoani Mara, Janeth Mayanja, amemsimamisha kazi mtumishi wa idara ya ardhi na mipango miji kwa tuhuma za kujipatia fedha kinyume cha sheria.

Akizungumza kwa simu mjini Bunda jana, Mayanja alisema alimsimamisha kazi mtumishi huyo, Eliud Haonga,  baada ya kudaiwa kutafuna Sh milioni tano, mali ya halmashauri hiyo.

“Juni 28 mwaka huu, Eliudi Haonga alipokea Sh milioni saba kutoka kwenye Kiwanda cha Olam ikiwa ni kodi ya pango kwa mwaka wa 2015/2016.

“Baada ya kuchukua fedha hizo  mtumishi huyo aliweka kwenye akaunti ya halmashauri ya mji Sh milioni mbili na kiasi kilichobaki, yaani Sh milioni tano,  alizichukua na kuzitumia kwa masuala binafsi kinyume na taratibu za utumishi wa umma.

“Kibaya zaidi, Haonga aligushi risiti ya halmashauri ya mji na kuikabidhi katika  Kiwanda cha Olam baada ya kupokea fedha hizo.

“Kwa hiyo  nimeamua kumchukulia hatua kwa mujibu wa kifungu namba 38 (1) cha kanuni za utumishi wa umma za mwaka 2003,” alisema Mayanja.

Ili kukabiliana na udanganyifu huo, Mayanja aliwataka watumishi wa umma katika halmashauri hiyo  kuwa waadilifu  wanapokuwa wakitimiza majukumu yao.

Kwa mujibu wa Mayanja, mtumishi yeyote atakayekiuka sheria za utumishi wa umma  atachukuliwa hatua   liwe fundisho kwa watumishi wengine wasiofuata maadili ya kazi zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,745FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles