26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Diwani kortini kwa kuhamasisha Ukuta

DIWANI wa Kata ya Sombetini, Ally Bananga (Chadema)
DIWANI wa Kata ya Sombetini, Ally Bananga (Chadema)

Na JANETH MUSHI, ARUSHA

DIWANI wa Kata ya Sombetini, Ally Bananga (Chadema), amefikishwa katika Mahakama ya Mkoa wa Arusha kwa tuhuma za kuhamasisha wananchi waandamane Septemba mosi, mwaka huu.

Bananga alifikishwa mahakamani   jana mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Agustino Rwizile.

Akisoma shtaka hilo, Wakili wa Serikali Charles Kagirwa, alidai mtuhumiwa  alitenda kosa hilo Agosti 13 mwaka huu wilayani Karatu.

Alidai   siku hiyo ya tukio, Bananga akiwahutubia wananchi katika mkutano wa wazi uliofanyika eneo la Hosteli ya Karatu, aliwahamasisha wananchi hao washiriki katika kusanyiko lisilo halali Septemba mosi mwaka huu.

Baada ya kusoma shtaka hilo, Wakili Kagwira aliiomba mahakama hiyo iahirishe kesi hiyo kwa kuwa upelelezi ulikuwa haujakamilika.

Katika shtaka hilo, Bananga anatetewa na Wakili John Mallya akisaidiana na Wakili James Lyatuu.

Mawakili hao kwa nyakati tofauti, waliiomba mahakama iruhusu dhamana kwa mshtakiwa yenye masharti nafuu kwa kuwa mtuhumiwa ni diwani anayeweza kujidhamini mwenyewe.

Hakimu Rwizile alikubaliana na ombi hilo na Diwani Bananga kujidhamini kwa dhamana ya Sh milioni tano.

Shauri hilo liliahirishwa hadi Septemba 22 mwaka huu, litakapotajwa tena.

Wakati shtaka hilo likitajwa mahakamani hapo, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema( Chadema), aliwaambia waandishi wa habari  kwamba maandamano ya Septemba mosi yanayolenga kupinga wanachokiita Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta), yako pale pale kwa kuwa maandalizi yake yanakwenda vizuri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles