26.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 26, 2023

Contact us: [email protected]

Risasi zarindima kesi ya kina Sheikh Fadrid

 Sheikh Farid Ahmed
Sheikh Farid Ahmed

Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

POLISI wameanza utaratibu mpya wa kupiga risasi juu kuwatawanya ndugu na jamaa waliofika kusikiliza kesi ya ugaidi inayomkabili Kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu (Jumiki) visiwani Zanzibar, Sheikh Farid Ahmed na wengine 63.

Hofu ilitawala jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kusikika milio ya risasi nje ya uzio wa mahakama na kusababisha taharuki kwa waliokuwa katika eneo hilo nje na ndani.

Milio hiyo ya risasi ilisikika jana saa tano asubuhi wakati watuhumiwa hao wakitoka mahakamani baada ya kesi zao kutajwa.

Mtanzania ilifuatilia tukio hilo kwa maafisa mbalimbali katika mahakama hiyo ambapo baadhi walisema walisikia milio wakiwa ndani lakini hawakujua ilitokea wapi.

“Wamepiga risasi juu walipotoka na hata asubuhi walipoingia walipiga risasi juu,”alisema mfanyakazi mmoja wa mahakama hiyo ambaye hakutaka kutajwa jina lake.

Afisa wa Polisi aliyekuwa katika msafara huo alipoulizwa kuhusu utaratibu huo mpya wa kupiga risasi juu, alisema walifanya hivyo kwa ajili ya kuwatawanya ndugu na jamaa waliokuwa wakisogelea basi la watuhumiwa.

“Tulipiga risasi juu kuwatawanya, kuna wale wanaokaa nje wanaimba takbir…takbir, tulipokuwa tunatoka walikuwa wanasogelea magari, unajua wakitusogelea wale wanatumaliza… si unaona wanavyotumaliza,”alisema askari huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,726FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles