Mkude ampa Aussems kigugumizi

0
726

Theresia Gasper -Dar es salaam

SAKATA la kiungo wa Simba, Jonas Mkude, kutojiunga na wenzake katika ziara ya Kanda ya Ziwa kwa ajili ya mechi mbili za Ligi Kuu Tanzania Bara, kimeendelea kumtia kigugumiza Kocha Mkuu wa timu hiyo, Patrick Aussems.

Mkude amejikuta matatani baada ya ya kukosekana katika safari ya kwenda Bukoba, mkoani Kagera wiki iliyopita tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar kabla ya kuifuata Biashara United, mjini Musoma, Mara.

Simba ilicheza dhidi ya Kagera Sugar Alhamisi iliyopita ambao walipata ushindi wa mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Kaitaba, kabla ya kuichapa Biashara United mabao 2-0, Uwanja wa Karume Mara, Jumapili iliyopita.

Juu ya sakata hilo, MTANZANIA lilitaka kufahamu Aussems analichukuliaje ambapo hakutaka kuzungumza chochote kuhusiana na mchezaji huyo.

“Siwezi kujibu swali hilo kwani kwa sasa naendelea na programu yangu ya mazoezi, huku nikiendelea kuwaandaa wachezaji wangu kwa mechi zinazotukabili mbele yetu,” alisema.

Katika hatua nyingine, Aussems alisema kwa sasa amebadili programu kwa wachezaji wake kuelekea mchezo wawao ujao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC, unaotarajiwa kuchezwa Octoba 23, mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Ili kujiweka fiti zaidi, kikosi hicho kinaweza kucheza mechi ya kirafiki na timu moja kutoka Kigoma kutokana na kuwa na muda mrefu wa kujiandaa kuwakabili Azam.

Wakati huo huo, kuna habari kuwa jana kikao cha cha Kamati ya Nidhamu kilikutana kwa ajili ya kujadili suala la Mkude, ambako leo kila kitu kinatarajiwa kuwekwa wazi kuhusiana na hatma ya mchezaji huyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here