29.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mkoa wa Geita kuendeleza ushirikiano na Waandishi wa Habari

Na Anna Ruhasha, Geita

Serikali mkoani Geita imeuhakikishia Umoja wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani humo(GPC ) kuendeleza ushirikiano nao katika kuhabarisha umma masuala mbalimbali ya maendeleo ndani ya mkoa huo.

Akizungumza kwa niaba ya mgeni rasmi ambaye alikuwa Mkuu wa Mkoa huo, Rosemary Senyamule katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari ambapo klabu ya waandishi wa habari mkoani Geita imeazimisha Mei 16, mwaka huu Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Said Nkumba amesema Serikali inatambua mchango wa waandishi wa habari ambapo amesema wataendelea kushirikiana nao kwa karibu.

Aidha, Nkumba ametumia siku hiyo kuwataka waandishi wa habari mkoani humo kupendana na kufanyakazi kwa ushirikiano pasipo kujiona bora kuliko wengine katika ufanyaji kazi wa kuhabarisha umma.

Baadhi ya washiriki katika siku hiyo akiwemo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, SACP Henry Mwaibambe amewaomba waandishi wa habari kuandika habari za uchunguzi hasa za matukio ya mauaji.

“Nimpongeze Mwenyekiti wa klabu yenu, Renatus Masuguliko kunatukio lilitokea la mauaji huko vijijini alilifuatilia kwa kina na habari yake pia ililisaidia jeshi la polisi, niwaombe pia wengine mchunguze kwanza kabla ya kuandika, japo ni baadhi tu ya waandishi ambao wanaandika bila kijiridhisha kwa kina,” alisema SACP MMwaibambe.

Upande wake, Renatus Masuguliko akizungumza kwa niaba ya wanachama amesema kuwa Chama cha waandishi wa habari kinachotambulika kwa mujibu wa sheria ni kimoja kwa mkoa wa Geita ambacho ni GPC, hivyo ameiomba mialiko inayotolewa na Serikali kwa wandishi ipitie katika ofisi hiyo.

“Mgeni rasmi tukuombe kunamialiko mbalimbali inatolewa lakini haipiti ofisini kwetu, klabu hii inatambulika na imesajiliwa kisheria na waandishi wananchama ni waandishi wenye sifa tuombe hilo lifanyiwe kazi,” amesema Masuguliko.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles