Mke wa Nipsey Hussle apewa mamlaka kamili

0
780

LOS ANGELES, MAREKANI

FAMILIA ya marehemu, Ermias Asghedom maarufu kama Nipsey Hussle, imempa mamlaka kamili ya uangalizi wa watoto (Guardianship) mke wa rapa huyo, Lauren London.

Nipsey ambaye alifariki dunia Machi 31, mwaka huu kwa kushambuliwa na risasi mjini Los Angeles, Marekani, alipata mtoto mmoja na mkewe, Lauren London anayeitwa Kross (3).

Katika hatua nyingine, Lauren ambaye pia ni mwigizaji amepewa nafasi ya uangalizi wa urithi wa mtoto, Kross, unaokadiliwa kuwa ni zaidi ya shilingi bilioni 2.2.

Kabla ya Lauren kuwa kwenye mapenzi na Nipsey, alibahatika kupata mtoto wa kiume na rapa Lil Wayne anayeitwa Kameron Carter huku Nipsey naye akiwa na mtoto mkubwa wa kike, Emani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here