Bonge la Nyau awatazama Kiba, Dully Sykes

0
987

Na GLORY MLAY

STAA wa Bongo Fleva, Lameck Jacob ‘Bonge la Nyau’, amesema  anafuata nyayo za wakongwe Alikiba na Dully Sykes kwa kutochora michoro ya mwilini maarufu kama tattoo.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Bonge la Nyau  anayetamba na wimbo wake mpya Kitochi, alisema anapenda kujulikana kutokana na kazi zake na siyo kuchora tattoo na kutoboa masikio kama wanavyofanya mastaa wengine.

 “Ali na Dully wanaimba vizuri na kazi zao zinatambulika hafanyi vibaya eti kisa hajatoboa masikio au hajachora tattoo, naamnini usafi unaanzia kwenye mwili,” alisema Bonge la Nyau.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here