26.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, January 18, 2022

MKAZI WA MABIBO AKIRI KUMUUA MWENZAKE

Na KULWA MZEE – DAR ES SALAAM

MKAZI wa Mabibo, Dar es Salaam, Jackson Mchaki, amekiri kumuua bila kukusudia Ramadhani Iddy, maarufu Mashine baada ya kugombana.

Mshtakiwa huyo alikiri kufanya mauaji hayo jana mbele ya Msajili wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Mustapha Siyani, aliyepewa mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Upande wa Jamhuri, ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Anna Chimpaye na Yasinta Peter, ulimsomea mshtakiwa mashtaka na maelezo ya awali ya kesi yake.

 Ilidaiwa kuwa Julai 4 mwaka 2013, eneo la Mabibo, jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alimuua Mashine bila kukusudia.

Mshtakiwa alikiri na mahakama ilimtia hatiani kwa kosa la kuua bila kukusudia.

Maelezo yaliyosomwa mahakamani hapo kuhusu tukio hilo la mauaji, yanadai kwamba mshtakiwa na Mashine walikuwa wanafahamiana.

Inadaiwa siku ya tukio, wote wawili walikuwa pamoja eneo la Mabibo. Walianza kugombana kwa kujibishana maneno, lakini watu waliokuwapo eneo hilo waliwaamulia na ugomvi uliisha.

 “Walipoamuliwa na ugomvi kuisha, baada ya muda walianza kugombana tena na mshtakiwa alichomoa kisu na kumchoma Mashine ambaye alianguka na kupoteza fahamu.

 “Watu walijitokeza kumsaidia na kumpeleka Kituo cha Polisi Urafiki kwa ajili ya kupata fomu namba tatu, lakini wakiwa njiani kwenda Hospitali ya Mwananyamala, alifariki,” ilidaiwa.

Jamhuri ilidai baada ya uchunguzi wa daktari kufanyika, ripoti ilieleza kwamba Mshine alifariki dunia kutokana na jeraha la kuchomwa na kisu.

Mshtakiwa baada ya tukio hilo alitoroka kwenda Mdaula mkoani Pwani ambako alijisalimisha Kituo cha Polisi Mdaula na alifunguliwa mashtaka ya mauaji.

Hukumu dhidi ya mshtakiwa huyo inatarajiwa kusomwa leo. 

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
174,926FollowersFollow
531,000SubscribersSubscribe

Latest Articles